Tabora tumepiga hatua katika Sayansi na Teknologia, ushahidi huu hapa....

Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,538
2,155
Wana JF,

Serikali ya CCM na uongozi imara wa viongozi wake wamepiga hatua kubwa na ya kusifiwa katika mkoa ambao ama ulisahaulika ama uliwekwa kiporo.

Katika pitapita zangu nimegundua maendeleo makubwa kabisa kutokea katika mkoa huu ambayo pia yalielezewa kwa kifupi katika taarifa ya miaka ya 50 ya uhuru na waheshimiwa viongozi wetu.

Tabora tumepiga hatua katika nyanja za utandawazi, ushahidi huu hapa. Fuata link hii;

TOVUTI YA MKOA WA TABORA

Asante.

Kassanga.
 
tabora bado sana japo ni mkoa wa zamani kihistoria kuliko hata dar es salaam

ukipita mitaa kama isevya, ipuli na mingine life tyte sana..labda kama maendeleo unayoyaongelea ni yale ya kunywa pombe ya asali na kucheza madisco vumbi hapo ntakuelewa
 
mkuu umekurupuka tu nawewe! kuna nini sasa hapo hicho kiwebsite?

eti "serikali ya nyinyiemu na uongozi imara" nya...........fu.
 
Wana JF,

Serikali ya CCM na uongozi imara wa viongozi wake wamepiga hatua kubwa na ya kusifiwa katika mkoa ambao ama ulisahaulika ama uliwekwa kiporo.

Katika pitapita zangu nimegundua maendeleo makubwa kabisa kutokea katika mkoa huu ambayo pia yalielezewa kwa kifupi katika taarifa ya miaka ya 50 ya uhuru na waheshimiwa viongozi wetu.

Tabora tumepiga hatua katika nyanja za utandawazi, ushahidi huu hapa. Fuata link hii;

TOVUTI YA MKOA WA TABORA

Asante.

Kassanga.

Hiyo tovuti imeshusha ugumu wa maisha?
 
gkasanga acha kudanganya watu. Kuna nini hapo kwenye hiyo Tovuti. kama huna la kusema si unyamaze tu. hata wewe tengeneza tovuti yako sasa hivi. Wewe mwenyewe umeikimbia Tabora kwa sababu ya shida zake
 
Kasanga,

Kwanza asante kwa kutuwekea hiyo LINK.

Hivi ni wewe Kasanga G. wa pale Misheni wilayani Sikonge? Kama ndiyo basi tuwasiliane.

Pia karibu kwenye FACEBOOK Group inaitwa Tabora Ndio Kwetu.

Pia kuna kigroup kingine kinaitwa Sikonge Developments.

Karibuni sana tuangalie jinsi ya kuweza kuunasua mkoa wetu wa Tabora hata kama kwa kuhamasisha watu wabadilike maana habari ni kitu aghali sana duniani.
 
TOVUTI...!, hivi sasahivi kuwa tovuti ni kiashiria cha kuwa maendeleo ya kisayansi ee..?
 
Tuonyeshe isevya,kiloleni,kanyenye,n'gambo kama zmechng 2takubal,unaposema tabora bla hzo sehem 2najua tabora wilaya zake.
 
Ha ha ha ha ha ha! Kumbe siku hizi Mlima Kilimanjaro uko Tabora? Ndio, najua huo mlima ni wa kitaifa lakini linapokuja suala la kimkoa usingepaswa kuonekana kama nembo kuu. Bora hata wangetuonesha miembe walikonyongewa akina Isike na maeneo muhimu Mwarabu (Tip Tippu, et. al) alikochinjia mababu zetu nyakati za utumwa.

By the way, hivi hiyo website ILIUNDWA kwa bei gani? Wala usitake kujua maana utazimia. Kwa haraka haraka hadi hapo ilipo isingepaswa kuzidi 250,000/= (ndio, laki mbili na nusu) lakini hukawii kuambiwa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI wali-spend more than 60,000,000/= ni jambo la kawaida sana kwa hii nchi. "Wajanja" walishachukua chao wamesepa; mtaendelea kuiona hivyo hivyo forever labda uje utawala mwingine lakini sio huu wa magamba.
 
Mikoa yote iliyokuwa nyuma kimaendeleo Kikwete kaifunguwa hususan, Tabora, Kigoma, Tanga, Mtwara.

Wana Tabora tunawatakia mafanikio mema na mtazidi kufaidika pale barabara kubwa za kuzunguka mkoa huo zitakapomalizika, zote zipo karika hatua mbali mbali za ujenzi. Ahsante Kikwete.
 
Du! aibu!! nimeangalia ukurasa wa barabara inaonyesha kuna jumla ya Km 5588.31 za barabara kati ya hizo zenye lami ni Km 158.6.Sikutaka wala kuendelea kuangalia kurasa nyingine.Sasa angalia hapo, mji mkongwe kama Tabora unazidiwa na mikoa kibao.Aibu tupu!!!!!!!!!!! Lazima mbadilike wana Tabora,Mmeonewa na kupuuzwa kiasi cha kutosha mnahitaji M4C kuuinua mkoa huo otherwise utabaki kuwa chini na chini zaidi!!!!
 
ebana naomba huu uwe utani ila kama kweli...kuna mdau anapenda kusema WEWE NI JINGAAA nimeenda tabora hali ni mbaya maisha ya watu hayatii moyo, barabara ya kwenda tabora kipande hata hakizidi km 10 unatumia masaa manne kufika kutokana na ubovu halafu magreda yamekaa tu sijui wanasubiri 2015 uchaguzi waanze kazi yaani bora kupanda treni halafu hawa jamaa sijui wamelishwa nn.....
 
Ni vigumu kunielewa ndugu yangu, hapo nimewakumbusha wajinga waliosema ktk report ya miaka 50 ya uhuru waache makelele kama yale ya tarehe 9 june pale jangwani, soma ktkt ya mistari acha kukurupuka kudandia hoja kaka. Maana yangu ni kwamba je huyo RC wa Tabora anakubaliana na utumbo huu? Hivi mimi ni zumbukuku wa kushabikia utumbo kama hui? Soma kwa maarifa, hiyo ni wakeup call kwamba tumeamka na tunafuatilia kila linalohusu mkoa wetu.

Nimezaliwa Tabora, nimesoma na kula huko, nimerudi Tabora kuwafumbua masikio Wanyamwezi waluosahaulika kwa mtindo kama huo. Kama hakuna wa kuwadhihaki CCM na ahadi kila kukicha je watahtuka? Nisome kwa maarifa utanielewa, acha ushabiki. Mimi ni CDM hai sina muda wa kusifia ujinga kama unaofanywa na watawala wetu, umeipata eehh?
gkasanga acha kudanganya watu. Kuna nini hapo kwenye hiyo Tovuti. kama huna la kusema si unyamaze tu. hata wewe tengeneza tovuti yako sasa hivi. Wewe mwenyewe umeikimbia Tabora kwa sababu ya shida zake
 
Wana JF,

Serikali ya CCM na uongozi imara wa viongozi wake wamepiga hatua kubwa na ya kusifiwa katika mkoa ambao ama ulisahaulika ama uliwekwa kiporo.

Katika pitapita zangu nimegundua maendeleo makubwa kabisa kutokea katika mkoa huu ambayo pia yalielezewa kwa kifupi katika taarifa ya miaka ya 50 ya uhuru na waheshimiwa viongozi wetu.

Tabora tumepiga hatua katika nyanja za utandawazi, ushahidi huu hapa. Fuata link hii;

TOVUTI YA MKOA WA TABORA

Asante.

Kassanga.

gamba la kobe ww! hivi unaongelea Tabora ipi? Tabora hii uenye cheyo,Kiloleni, Ng'ambo, mwinyi etc, bila shaka ww utakua umevuta kidogo kitu kutoka kwa Rage. eboo ..!
 
Ndio mimi hasaa, cheki nami at godfrey120@hotmail.com au call 0786546555, sina cha kuficha.

Back
Top Bottom