TUSHIRIKISHANE TABORA: Timu ya JamiiForums yapata ajali maeneo ya Mbaoni - Urambo

TAARIFA​

Tunasikitika kutangaza kutokea kwa ajali ya timu (2) ya wana Jamii Media, waliopo kwenye safari za mradi wa TUSHIRIKISHANE (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") iliyotokea hapo jana saa 5 asubuhi, maeneo ya Mbaoni - Urambo (Tabora). Timu hiyo ilikuwa na Meneja Uendeshaji na Mikakati wa Jamii Media, Bi Asha D. Abinallah na Mshauri wa Miradi Bw. Ericus Kimasha.

Timu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.

Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.

View attachment 383076

View attachment 383075

View attachment 383077
View attachment 383135Jamii Media inawashukuru Sana Bw. na Bi. Banyanga, wamiliki wa Magole Pre & Primary School kwa kuwasaidia wafanyakazi wetu waliopata ajali
View attachment 383136
Jamii Media inawashukuru Afande Jonas na Afande Abdallah wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilayani Urambo kwa msaaada na huduma ya haraka kwa wafanyakazi wetu.

JamiiForums​
Du!
Poleni sana.
Sehemu ni nzuri tu ya ajali, sababu ni nini?
Aidha
  1. Mwendo kasi, ruts (vituta vya kuudhi barabara za udongo hupokonya usukani)
  2. Kupasuka tairi
  3. Dereva usingizi
Haya ni majumuisho yangu ya safari zangu nyingi mikoani.
Hata hivyo ni vema kumshukuru Mungu it could have been much worse.
 
Poleni sana wenzetu
Lakini Simu nyingine mkija msitusahau nasisi wa Wilaya ya uyui japo jiografia ya Wilaya hii ni mbaya basi tunaweza kutana hata tabora mjini
 
Dah,poleni sana wapambanaji wetu. Katika utekelezaji wowote ule hua mikosi haikosekani ichukulieni kama mitihani tu. Mungu awanusuru daima ameen.
 
TAARIFA​

Tunasikitika kutangaza kutokea kwa ajali ya timu (2) ya wana Jamii Media, waliopo kwenye safari za mradi wa TUSHIRIKISHANE (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") iliyotokea hapo jana saa 5 asubuhi, maeneo ya Mbaoni - Urambo (Tabora). Timu hiyo ilikuwa na Meneja Uendeshaji na Mikakati wa Jamii Media, Bi Asha D. Abinallah na Mshauri wa Miradi Bw. Ericus Kimasha.

Timu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.

Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.

View attachment 383076

View attachment 383075

View attachment 383077
View attachment 383135Jamii Media inawashukuru Sana Bw. na Bi. Banyanga, wamiliki wa Magole Pre & Primary School kwa kuwasaidia wafanyakazi wetu waliopata ajali
View attachment 383136
Jamii Media inawashukuru Afande Jonas na Afande Abdallah wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilayani Urambo kwa msaaada na huduma ya haraka kwa wafanyakazi wetu.

JamiiForums​
Poleni mkuu, Mungu awafanyie wwpesi.
 
Back
Top Bottom