Tabora: Polisi kuanzisha msako wa wanaotaka kujinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani

Awamu hii full comedy sio rc sio dc sio RPC sio OCD afadhari labda IGP kidogo ameweza kujizuia kuwa kituko
 
Kuna kesi nyingi zitafuata baada ya Utakatishaji , Uhujumu na hatimaye hii ,hii sasa itaenda na wengi ,sharti
Usibebe kamba kama huna pakuifunga
Usinunue vidonge kama huumwi
Usinunue sumu ya aina yoyote iwe yakuua wadudu au wanyama kama huna sehemu rasmi pakuitumia.
Wale wote wenye stress/msongo wa mawazo mchukue tahadhari, 2020 ni mwendo wa gereza

Vioja mahakamani @ new episode

Cc:watakatishaji
 
.
Swala siyo kumshtaki bali ni namna ya kumbaini mtu mwenye kusudio la kujiua na kumdhibiti maana kama yeye anataka kujiua atashindwaje kujiua wewe unayetaka kumpokonya kamba yake
Ushahidi utalenga mambo gani? Hapa ndugu Mshana Jr changamkia fursa unaweza kuwa wakili upande wa Jamhuri ama kusimama kama mpelelezi kabisa wa kutafuta viashiria kwa kutumia elimu yetu ileeee ya kusoma nyota! Asante!
IMG-20200103-WA0134.jpeg

Jr
 
Mimi namsubiri atakayetoa tamko la kuwakamata wote wenye dalili za kubaka ama kuchepuka
Nasubiri mkuu wa polisi wa ule mkoa ambao mapenzi ndipo yalipozaliwa naye kesho aandae press conference atangaze kuwatia ndani watu wote wenye jinsia ya kiume ambao hawajaoa!

Jr
 
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Barnabas Mwakalukwa amesema kufuatia kupokea taarifa ya watu wawili kujinyonga, mwaka huu wataanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga

Amewakanya wanaotegemea kujinyonga kuwa tabia hizo zikome kwani wao wataanza kufanya doria na kuwakamata kabla hawajajinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani

Ameongeza, “Tunaomba viongozi wa Taasisi za Kiroho wafanye doria za Kiroho za kuzima matukio ya namna hiyo kwa kutoa nasaha, elimu na Wataalamu wa Afya waende kwe wagonjwa wenye matatizo ya akili ili wawape faraja kuwa bado wana nafasi ya kuwa na maisha bora.”

Amesema wakati mwingine tunapoteza Wataalamu ambao wangesaidia nchi yetu. Amesema “Tumepoteza Mwalimu, Mjasiriamali labda hawa baada ya miaka miwili wangekuwa Maprofesa au matajiri wa Afrika.”

View attachment 1310964
...Serious? 'Msako Wa WANAOTAKA kujinyonga? Eh?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo rpc akili zake kama za jiwe yani kilaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom