KIPUMPUSWA
Senior Member
- Jul 16, 2011
- 106
- 35
Ofisi ya mkuu wa mkoa tabora imesambaza waraka ukiwaelekeza wafanyakazi wote mkoani hapa kushiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa tanganyika. Waraka huu unasambazwa na kikundi cha watu wasiopungua 8 pia wanajeshi wapo. Wanapofika ofisi, mkuu wa ofisi anatakiwa ataje idadi ya wafanyakazi wake, idadi hiyo kuandikwa katika kitabu.Para ya mwisho wa waraka huo inasomeka hivi ,ni lazima wafanyakazi wote katika taasisi yako washiriki katika maandamano hayo. Mfanyakazi ambaye hatohudhuria maandamano hayo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.Wakuu mliopo tabora najua waraka huu mmeupata.