Habari wana jamvi. mimi niko Tabora, lakini kitu cha ajabu mji mzima kumejaa mabango ya waganga wa kienyeji, ambayo yanashawishi wananchi kufanya vitendo vya uhalifu. Swali langu ni hivi, hakuna viongozi wa mitaa? na ni nani anatoa ruksa kubandika mabango haya kwenye nguzo za Tanesco? mimi binafsi inanikera na sipendi sana.