Tabora: Mzee auawa kisa mgogoro wa ardhi, watano mbaroni wakihusishwa na mauaji hayo

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,101
JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kumuua mkazi na mkulima wa kijiji cha Wita, Kata ya Ndala Wilaya ya Nzega mkoani hapa, Andrea Kipela (72) chanzo kikiwa ni mgogoro wa ardhi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kati ya wananchi wa kijiji hicho na Kamati ya Ulinzi ya mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Laurian Fabrian alisema wanawashikilia watu watano kuwahoji.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na majina ya watuhumiwa yamehifadhiwa kwa ajili ya kuwapata wengine wanaohusika na mauaji.

Mwanri amesema wale wote watakaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo, serikali ya mkoa haitasita kuwachukulia hatua zaidi za kisheria.

“Serikali kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama inawaomba wananchi kutoa taarifa za watakaodaiwa kuhusika na mauaji,” alisema.

Ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa na Wilaya ya Nzega kuwalinda wanafamilia wa marehemu Kipela kipindi hiki ili wasidhurike kwa lolote lile wakati upelelezi ukiendelea.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Robert Makungu na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula walisema watailinda familia na kuwataka wananchi kuwa walinzi wa kwanza wa familia hiyo na wanafamilia kujilinda pia.

Awali akizielezea ekari za ardhi zilizokuwa na mgogoro huo na kusababisha kifo cha Kipela, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Yahaya Sekiete alisema zipo ekari 180 na zilikuwa hazijapimwa na baada ya mavuno zitapimwa na kukabidhiwa kwa wanafamilia.

Ekari hizo zinatambuliwa na Mahakama ya Ardhi licha ya Kipela kushinda kesi hiyo ya mgogoro wa ardhi iliyokuwa mahakamani.

Kipela aliuawa Februari 2 mwaka huu huku chanzo cha kuuawa kwake ikiwa mgogoro wa ardhi ya kulima katika kijiji hicho cha Wita.
 
Back
Top Bottom