Tabora: Mwanafunzi afungwa jela miaka 20, akutwa akiwaonesha wanafunzi picha za ngono kupitia simu yake ya mkononi

Hakimu kakosa busara, miaka 20 ni mingi sanaa, na judgement yake kaifanya kwa hisia labda uenda nae ni mzazi nae.
Jaribu kufuatilia hukumu zinazotolewa mahakama za chini mkuu. Kuna kitu hakiko sawa, mara nyingi hua zinatoka hukumu za juu mno.
 
Yaani kuwachezea sehemu za siri na wao kuchezea ni kosa dogo ambalo lahitaji kuomba radhi kweli? Kwani kwenu kosa kubwa ni lipi?

Acha kuchukulia mambo rahisi kiasi hicho Mkuu. Angalia upande wako kuwa kama wanao amefanywa hivyo ungejisikiaje?
Labda yeye ameshazoea kuchezewa ndio maana anachukulia poaa,. Watu tunafikiria kukuza viwanda kiuchumi yeye yuko busy kuzalisha mapunga.. Shwain kbsa huyo mimi ningemfanyia operation ya kuondoa hicho kidudu chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wamemuonea kosa lake ni dogo na adhabu ni kubwa... kuonesha video zilizoruhusiwa kuingia nchini sio kosa mamlaka husika zinatakiwa kuzuia.. uonevu kwa wanyonge bado unaendelea mikoani kuna wanaojifanya viduduwatu. Huyo denti alitakiwa aombe radhi tu pekee
Kuwa na aibu!!
Kuchezewa nyeti na watoto ni kosa dogo??
Akitoka hapo ataanza kuwaingilia watoto wa watu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Tawi la Tabora Marick Mbega amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya kuwadhalilisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Isike mkoani hapa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, Emmanuel Ngigwana alitoa adhabu hiyo juzi baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka wakiwamo wanafunzi waliodhalilishwa.

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Upendo Malulu uliieleza Mahakama kuwa Mbega alitenda makosa hayo Aprili 4 mwaka huu, kinyume na kifungu namba 138 A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya 2002.

Wakili Malulu alidai siku hiyo katika eneo la Shule ya Msingi Isike katika Manispaa ya Tabora, mshtakiwa alikutwa akiwaonesha wanafunzi picha za ngono kupitia simu yake ya mkononi.

Alisema mbali na Mbega kuwashawishi wanafunzi hao wamshike sehemu za siri, pia alikuwa akiwachezea.

Wakili Malulu alisema baada ya kufanya upekuzi katika simu ya mshtakiwa, ilikutwa ikiwa na picha 197 za ngono na video 40 zikiwamo za watoto, watu wazima na wanyama.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu Ngigwana alisema mtu anayeonyesha sehemu zake za siri, kuchezea za watoto, kuonyesha picha za ngono au filamu za ngono anafanya udhalilishaji na ni kinyume cha sheria.

Alisema mtoto hana uamuzi kisheria, hivyo hawezi kuchukuliwa kwamba alikubali matendo hayo.

Hakimu Ngigwana alisema Mahakama imeona mashtaka ni mtu mzima tena Mwanafunzi wa Chuo cha Umma aliyedhaniwa kuwa na maadili kwa jamii, mstaarabu, mwenye kujali, kulinda na kutetea maslahi ya watoto, lakini alitenda kosa hilo, hivyo anastahili adhabu.

Pia, alisema mshtakiwa alipaswa kuhakikisha mtoto anakuwa vizuri kiakili, kimwili, kiroho na kisaikolojia badala yake amekwenda kinyume.

Alisema ili iwe fundisho kwake na onya kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo, atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka kumi jela kwa kila kosa.

Chanzo: Mwananchi
:eek::eek::eek::eek: hao ndo wasomi wetu...anyway mahakimu nao hii ni aibu mtu anaiba billions mnashindwa kumfunga lkn anayehitaji ushauri ndo mnampa mpaka adhabu za wengine...kisa tu ni maskini
 
mkuu siku hizi kuwa picha hizo kwenye simu sio issue watu wanazo zaidi ya hizo tena wengine wanaheshimika sana, kwenye lap top ndo usiguse huko ni balaa, mambo yale sio mchezo. Ila hilo la kuvamia vitoto kama babu seya halikubaliki kamwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ni matatizo ya kisaikolojia.

Wewe na akili timamu unaweza kuwa na video za binadamu akifanya mapenzi na wanyama?? Au video za watu wazima wakiwabaka watoto???

Video za ngono 40????
 
:eek::eek::eek::eek: hao ndo wasomi wetu...anyway mahakimu nao hii ni aibu mtu anaiba billions mnashindwa kumfunga lkn anayehitaji ushauri ndo mnampa mpaka adhabu za wengine...kisa tu ni maskini
Ni kweli wezi hawafungwi nchini. Ila huyo hastahiki ushauri, bali ni adhabu hata kama si miaka 20 basi walau chini ya miaka mitano
 
Back
Top Bottom