Tabora: Mwalimu mbaroni kwa kujifanya Askari Polisi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,312
2,000
Polisi mkoani Tabora inamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi Shila wilayani Nzega, Ferdinand Felix (33) kwa tuhuma za kujifanya polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema leo Jumatatu Mei 5, 2019 kuwa mwalimu huyo alikamatwa juzi saa 3:00 asubuhi katika baa na nyumba moja ya kulala wageni.

Amesema polisi walipata taarifa kuwa kuna tapeli anayedai kuwa ni askari kutoka Kituo cha Kasulu mkoani Kigoma na kwamba yupo likizo wilayani Nzega.

Nley amesema mtu huyo alipotakiwa kuonyesha kibali maalumu kinachomtambulisha maarufu kama movement order, alishindwa kukionyesha hivyo kudai kuwa yeye ni mwalimu.

Amesema uwapo wa soko la madini Nzega umevutia wahalifu na matapeli ambao wanataka kujipatia fedha kwa njia haramu.

Amewataka wakazi wa Nzega kuwa makini na matapeli hasa baada ya kuanzishwa soko la madini kwenye wilaya yao.

Diwani wa Nzega Mjini Mashariki, Frederick Ruhangisa, amesema matapeli wamekuwa wakisumbua hata kabla ya kuanzishwa soko la madini.

Amesema matapeli hao wamekuwa wakiwasumbua wananchi hasa katika mtaa wa Benki ya NMB na tayari wamejiwekea utaratibu wa kuwapa tahadhari wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
 
Mkulubilanga

Member
Sep 23, 2013
40
95

Hapo hakuna ushaudi wowote unaonesha yeye ni taperi mtu anayo kazi yake halali unamwita taperi tatizo liko wapi
 
Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,528
2,000
Aachiwe akafanye kazi yake ya ualimu tuna uhaba wa walimu..Madhari hakuna aliyelalamika kutapeliwa na huyo mwalimu.
 
Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
4,489
2,000
Labda ilikuwa gia yake ya kuwatongoza hao wahudumu,nina wasiwasi na huyo mwalimu ni domo zege.
Yaani anaona akijitambulisha yeye ni polisi nayo ni kazi ya prestige?!?
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
14,151
2,000
Mtu yuko bar mnamkamata mnajuaje labda pombe ndo zilimtuma hivyo? Au alisema yeye ni police jamii? Au aliona demu mkali akaja na gia ya upolisi,

hivi nikilewa nikasema mie ni trump nitakamatwa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom