TABORA: Mtu mmoja afariki baada ya kupokonywa hirizi zake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
Michael Paschal mwenye umri wa miaka 33, mkazi wa Uhemeli Ndala, Nzega, mkoa wa Tabora, afariki baada ya kuporwa hirizi zake na polisi akifanyiwa upekuzi.

Kijana huyo ambaye ni bodaboda alifikishwa kituoni mara baada ya kumkaba na kumchania sare CPL Lucas aliyekuwa katika majukumu ya usalama barabarani.

Askari (Lucas) alipomsimamisha Michael akiwa anaendesha pikipiki yenye usajili MC.246 BXH kwa ukaguzi, Michael alifanya fujo kwa kumkaba polisi na kumchania sare zake.

Askari alifungua mashtaka ya kuzuiwa kufanya majukumu yake, kijana Michael alikamatwa na kufikishwa kituoni alipokuwa akifanyiwa upekuzi alikutwa na hirizi mbalimbali sehemu ya mwili wake.

Mtuhumiwa akaomba asitolewe hirizi zake kwani zikitolewa atakufa, kulingana na sheria za upekuzi kwa mtuhumiwa anayewekwa mahabusu walizitoa hirizi hizo.

Baada ya kuzitoa hirizi hali yake ikaanza kubadilika kwa kuishiwa nguvu na kuzilai alipelekwa zahanati ya Kashishi kwa matibabu ilipofika saa 3.00 usiku akafariki dunia. Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora.
 
Mmmh polisi wetu hawa kweli tena kwa maelezo kuwa alikorofishana nao!! Hapo lazima kachezea kipigo kweli akawa hoi mpaka mauti sasa sababu iwe ipi ili wajinasue katika kumpekua wakagundua alikuwa na powerbank ya asili na kwa kuwa wengi wanaamini hayo ikabidi watokee huko.
 
Inamaana alivyochana gwanda hakufanywa chochote? nahisi alipewa mkong'oto hawezi kuchana akaachwa tu! Hirizi is by the way ila watakuwa walimwonyesha cha mtema kuni.
 
Sidhani kama kuna bodaboda hapo Uhemeli Ndala, Nzega, mkoa wa Tabora atamchania tena "trafiki" nguo zake za kazi!
 
Hapo polisi wameamua tu kwa makusudi kuhamisha magoli. Huenda walimpiga huyo mtuhumiwa kwa kitendo cha kumshambulia mwenzao! Baada ya kumjeruhi na kuona hali yake ni tete, wakaona bora watafute tu hicho kisingizio cha hirizi.
 
Back
Top Bottom