Tabora Mjini hakuna Maji kwa siku ya tisa mfululizo

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
Ni Mwezi umepita sasa tangu Prof kitila Mkumbo ahudhurie utiwaji saini wa mradi wa maji toka ziwa victoria kwenda mkoani Tabora.

Mkataba ulisainiwa mbele ya umma wa wana Tabora viwanja vya chipukizi.

Leo mji upo kwenye ukame,huduma ya maji imetoweka kwa madai ya Pump kuharibika.

Inamaana hiyo pump inauzwa mil mia ngapi hata Mamlaka inatokusanya mamilioni kushidwa kuwa na Pump ya akiba?

Kama pump ya Akiba ipo inachukuwa muda gani kuwa replaced na kuweka hiyo inayofanya kazi?

Kila mwezi wananchi wanalipia service charge isiyopungua 4000 kwa kila mtaji bila kujali kama maji yametoka au la.sasa kama service zinakusanywa zinafanya service gani hata kushindwa kurejesha huduma katika hali yake ya kawaida?

Hii wizara inaongozwa na Prof Kitila mkumbo kama Mkuu wa rasilimali watu wa wizara.

Tuulizie Meneja wa TUWASA anasubiri nini kuendelea kubaki ofisini wakati kazi anayolipiwa mshahara kashindwa kuifanya?

Tuwasa Itoshe kuwa mtihani wa kwanza kwa katibu mkuu mpya.
 
Huo mkoa kwa shida ya maji siuwezi japokua kuna maeneo hayasumbui lkn maeneo mengi maji ni shida
 
Misri, Sudani na Ethiopia wanaendelea kwa kupitia miradi ya bonde la mto Nile lakini sisi tuko busy kupokea msaada wa magari mawili ya taka
What a shame:eek::eek::eek:
 
Ni Mwezi umepita sasa tangu Prof kitila Mkumbo ahudhurie utiwaji saini wa mradi wa maji toka ziwa victoria kwenda mkoani Tabora.

Mkataba ulisainiwa mbele ya umma wa wana Tabora viwanja vya chipukizi.

Leo mji upo kwenye ukame,huduma ya maji imetoweka kwa madai ya Pump kuharibika.

Inamaana hiyo pump inauzwa mil mia ngapi hata Mamlaka inatokusanya mamilioni kushidwa kuwa na Pump ya akiba?

Kama pump ya Akiba ipo inachukuwa muda gani kuwa replaced na kuweka hiyo inayofanya kazi?

Kila mwezi wananchi wanalipia service charge isiyopungua 4000 kwa kila mtaji bila kujali kama maji yametoka au la.sasa kama service zinakusanywa zinafanya service gani hata kushindwa kurejesha huduma katika hali yake ya kawaida?

Hii wizara inaongozwa na Prof Kitila mkumbo kama Mkuu wa rasilimali watu wa wizara.

Tuulizie Meneja wa TUWASA anasubiri nini kuendelea kubaki ofisini wakati kazi anayolipiwa mshahara kashindwa kuifanya?

Tuwasa Itoshe kuwa mtihani wa kwanza kwa katibu mkuu mpya.

Haya ya ubovu wa miundo mbinu na uhaba wa maji kwa Tabora ninaona ni suala la kwanza.

Suala la pili ni uchafu wa huduma za maji ya matumizi ya binadamu.
Hii idara ya maji (Tuwasa), ninadhani ni idara ya kwanza nchini Tz kufanya huduma mbovu kiwango cha kutisha kwa kusukuma maji toka vyanzo vyake bila ya kuyasafisha na kuyatibu. Sijapata kuona mahali pengine popote maji yakisukumwa na kutumiwa na watu bila ya kusafishwa.

Ukiona bomba linatoa maji meupe,fuatilia vyombo vya habari, utakuta kuna ziara ya kiongozi flani anakuja.

Ama "kuzugia" mara mbili tatu kwa mwezi, mwendo wa funika kombe. Siku zingine ni kusukuma maji machafu kuhudumia wananchi bila kujali.

Hubaki kujiuliza hivi matendo yafanywayo na hii idara ya maji mkoani Tbr, hakuna kiongozi yeyote anayeona uozo huu nakuukemea?

Uozo huu wa idara ya maji umekuwa ni donda ndugu kwa muda mrefu sasa bila hatua zozote kuchukuliwa. Idara imekuwa ni kijiwe cha ulaji wa pesa za watu kwa huduma mbovu za maji machafu.

Ifike mahali sasa, wananchi wa Tabora, tuseme "no" kwa huduma mbovu zitolewazo na idara ya maji hii isiyojali afya za watu.

Viongozi wa idara, wapo miaka nenda rudi wakifumbia macho uozo huu, wala hawashituki.

Viongozi wa Wizara wapo, lakini suala hili la uzembe uliokithiri, kwao siyo tatizo.
Kama idara hii imeshindwa kuhudumia Tabora, iwajibishwe.
 
ndio miaka 55 ya ccm hiyo. kidumu chama cha ccm

maendeleo ya viwanda yatachukua muda kutimia kama maji ya matumizi ya majumbani tu ni kero kupatikana .....

umeme na maji ishakuwa kero, kweli wale wagosi wa kaya waliona mbali
 
Mbunge wenu anachekelea adhabu za kina Mdee, komaeni tu wakuu
 
Ni Mwezi umepita sasa tangu Prof kitila Mkumbo ahudhurie utiwaji saini wa mradi wa maji toka ziwa victoria kwenda mkoani Tabora.

Mkataba ulisainiwa mbele ya umma wa wana Tabora viwanja vya chipukizi.

Leo mji upo kwenye ukame,huduma ya maji imetoweka kwa madai ya Pump kuharibika.

Inamaana hiyo pump inauzwa mil mia ngapi hata Mamlaka inatokusanya mamilioni kushidwa kuwa na Pump ya akiba?

Kama pump ya Akiba ipo inachukuwa muda gani kuwa replaced na kuweka hiyo inayofanya kazi?

Kila mwezi wananchi wanalipia service charge isiyopungua 4000 kwa kila mtaji bila kujali kama maji yametoka au la.sasa kama service zinakusanywa zinafanya service gani hata kushindwa kurejesha huduma katika hali yake ya kawaida?

Hii wizara inaongozwa na Prof Kitila mkumbo kama Mkuu wa rasilimali watu wa wizara.

Tuulizie Meneja wa TUWASA anasubiri nini kuendelea kubaki ofisini wakati kazi anayolipiwa mshahara kashindwa kuifanya?

Tuwasa Itoshe kuwa mtihani wa kwanza kwa katibu mkuu mpya.
Muache dk ale kwanza bata jameni
 
Siku nane hakuna maji. Hao wanawake wamesurvive vipi ? Siji huko mpaka maji yapatikane
 
Back
Top Bottom