Tabora: Mganga wa jadi afariki akinadi kinga yake dhidi ya sumu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
660
1,000
Mtu mmoja ambaye amebainika kuwa ni mganga wa jadi, Robert Masumbuko, amefariki dunia mkoani Tabora wakati akijaribu kuwaaminisha wateja wake kwamba ana uwezo wa kuwapatia kinga dhidi ya sumu yoyote ambayo mtu anaweza kuinywa pasipo kudhurika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaonya wananchi kuepukana na dhana potofu ambazo zinaendelea kumshamiri kwa baadhi ya wananchi. Mtu huyo mkazi wa Kigoma lakini amefariki akiwa Kaliua mkoani Tabora.

Kwa msaada wa Azam
 

Black belts

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,423
2,000
Tatizo la wahaha wanajifanya wanajua kila dawa ya kila kitu,,

Juzi nilikuwa napiga pombe na muha mmoja pale WhatsApp pub Tegeta.

Alikuwa ananiambia yeye ana uwezo wa kuyeyuka ghafla na akaibukia kwao Kigoma, nikamjibu hauwezi acha uongo. Mara akawa anatafuta mtu mwenye sarafu ya mia mbili ampe ili afanye ivyo......
 

NDORANGA

Member
Feb 6, 2021
92
150
TatIzo la wahaha wanajifanya wanajua kila dawa ya kila kitu,,

Juzi nilikuwa napiga pombe na muha mmoja pale WhatsApp pub Tegeta,,

Alikuwa ananiambia yeye ana uwezo wa kuyeyuka gafla na akaibukia kwao kigoma,, nikamjibu hauwezi acha uongo,,
Mara akawa anatafuta mtu mwenye sarafu ya mia mbili ampe ili afanye ivyo......
Hahahahahah
 

CHIEF WINGIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2013
1,250
2,000
Hivi alidhani wazee wa Tabora watamwacha afanye mazindiko yake hadharani bila ya kumjaribu, hapo wazee wamemchapa kijini kimoja tu mganga chali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom