TABORA: Mfanyabiashara apigwa risasi na majambazi mchana kweupe

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mkazi wa Mpera, Mkoa wa Tabora, Mohamed Mustafa amefariki dunia kwa kupigwa risasi nyumbani kwake.

Mustafa ambaye ni mfanyabiashara wa asali amefikwa na mauti juzi Alhamisi Julai 14, 2022, akiwa anatoka nyumbani kwake kwenda kwenye shughuli zake za bishara.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao, akizungumza na Mwananchi, leo Jumamosi Julai 16, 2022 amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo na wanawashikilia watu wawili.

Mmoja wa jirani wa mfanyabiashara huyo, aliyeomba hifadhi ya jina lake amesema watu waliohusika na mauaji hayo walikimbia baada ya kumpiga risasi wakiwa umbali wa mita zipatazo hamsini.

"Mwenzetu alikuwa akienda kwenye shughuli zake na ndipo alipopigwa risasi akiwa anatoka nje ya nyumba yake," amesema jirani huyo

Naye mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Maulid Shaban amesema alipopata taarifa za tukio hilo alikwenda Hospitali ya Kitete na kukuta madaktari wanamshughulikia lakini baadaye akaambiwa amefariki.

Marehemu alikuwa anajishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ya asali na wanaomfahamu vyema wanasema alikuwa anakusanya asali kutoka maeneo mbalimbali na kuyahifadhi nyumbani kwake.

Inaelezwa marehemu alikuwa na fedha taslimu Sh16 milioni na watekelezaji wa tukio hilo hawakuchukua kitu chochote zikiwemo fedha hizo.
 
Ujambazi/wizi hapo sio motive. Hao sio majambazi.

Ni wauaji.

Polisi fanyeni kazi hapo kwa weledi mkianza na watu wake wa karibu (familia na wapinzani wake wa biashara) hafu mje mahusiano yake kama anatembeaga na wake za watu au nini.
Mambo ya biashara acha tu, ukikuta watu wana greedy kupotezana nje nje
 
uchunguzi utabaini sababu haswa ya kuuwawa, lkn kwa sasa sababu ya usaliti, kama vile kutembea na mke wa mtu inaongoza kuwa sababu ya mauaji.
 
Nilisikia ni story ya kudaiyana sasa sijui marehemu ndio alikuwa anadaiwa hataki kulipa au ndiye alikuwa anadai
 
Huyu atakuwa ametapeli wenzake. Duniani kuna watu wana viburi na dharau sana.
Anakudhulumu hela halafu anakuambia fanya chochote unachoweza. Si anajua huwezi mfanya chochote.
Kuna kenge mmoja, naye namsubiria ajae. Ndiyo ataisoma namba huyu. Huwezi kula hela ya mwanaume kirahisi hivi
 
Back
Top Bottom