John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia Maiko Jacobo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Kijiji cha Upungu, Wilaya ya Nzega mkoani hapo kwa tuhuma ya kutenda kosa la kumuua baba yake mzazi mzee Jacobo Lubela mwenye umri wa miaka 88 baada ya kumvizia majira ya jioni akiwa nje ya nyumba yake na kumkata shoka kichwani, shingoni na mikono yote miwili.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi wa Polisi, Richard Abwao amesema tukio hilo lilitokea Februari 28, 2022 majira ya saa 1 jioni ambapo mtuhumiwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa ambao amekuwa akiuhusisha kulogwa na baba yake mzazi.
“Mzee Jacobo alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo, akakimbizwa katika Hispitali ya Misheni ya Ndala, hali yake ilikuwa mbaya na akafariki usiku wa tukio, pia mtuhumiwa alimjeruhi ndugu yake mwingine Magdalena Jacobo ambaye alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka.
“Mtuhumiwa amekiri kuhusika na mauaji hayo na alikutwa na shoka aliyoitumia. Nitoe wito kwa wakazi wa Tabora kuacha kuwa na Imani za kishirikina ambazo zinasababisha matatizo kama haya,” anasema ACP Richard Abwao.
Source: Wasafi Digital