Tabora: Baba na mtoto wadaiwa kumuua mama kwa kuchoka kumuuguza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa kata ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyonga.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora ACP Sophia Jongo amesema tukio hilo limetokea Agosti 4, 2021 katika kijiji cha Isalalo tarafa ya Puge ambapo baba na mtoto wake wanatuhumiwa kumuua na kutengeneza tukio la kujinyonga.

Malunde blog
 
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa kata ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyonga.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora ACP Sophia Jongo amesema tukio hilo limetokea Agosti 4, 2021 katika kijiji cha Isalalo tarafa ya Puge ambapo baba na mtoto wake wanatuhumiwa kumuua na kutengeneza tukio la kujinyonga.
 
Wajiandae kunyongwa na wao,Hizo nguvu walizotumia kumuua huyo mama si bora wangetumia kukimbia wamuache akiwa hai Mungu angemtetea
 
Wengi sana tunaua ndugu zetu kwa kigezo cha sina pesa ya matibabu....halafu akifa unatoa ela nyingi za msiba.

Jichunguze kwako kama una mgonjwa ambay humuhudumii ipasavyo...(kwa maelezo ya dr) nawe ni muuaji
 
Mhhh huu ni ukatili sasa; wamebeba dhambi ya mauaji

ni mara kumi wangemtelekeza kuliko kumnyonga
 
Huyo mtoto ana uhusiano gani na huyo mwanamke? Bibi yake au mama yake
 
Roho nyingine ni za kishetani kweli! Wamechoka kumuuguza kwani wao ni Madaktari au Manesi?

Kwa nini wasingempeleka hospitali na kumtelekeza huko kama kweli walichoka kumuuguza!
 
Jamani,unamuuwaje mama yako mzazi tena bila woga kwa kuchoka kumuuguza. Malezi yalivyo na kazi, watoto mpaka kukua ni changamoto kwenye ukuaji leo mtu anamuua mama aliemkuza bila woga????....very sad!!!
 
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa kata ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyonga...
Ahaaaa ni Tabora kumbe nao Wanaua Wake zao!!!! Nilizani ni wale tuu ndio Wanaua. Huyu mtuhumiwa kuua mke Kabila Gani?
 
Kama alikuwa anaumwa kulikuwa na haja gani ya kuning'iniza juu bora wangemwacha tu kitandanai
 
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa kata ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyong...
AMINI HIZI NI NYAKATI ZA MWISHO,WATU WATAJIPENDA NA KUPENDA PESA KULIKO KUMPENDA MUNGU.
 
Uko sawa kweli?
Baba unauawa tu, kwanza Baba wengi wamepata watoto kwa kubaka wanawake,wengine kutokana na starehe zao na wengine wametelekeza watoto wao.Sasa kwa nini usiuawe?

Kuwa baba siyo kumwagia ndani bali ni kutoa malezi kwa mtoto,Mama yake pamoja na kuheshimu wanawake.
 
Back
Top Bottom