Tabora: Baba aua Mkewe na Watoto wawili kwa mchi wa kutwangia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za mauaji ya mkewe na watoto wawili wanaodaiwa kuuawa kwa kupigwa kichwani na mchi wa kutwangia kisha miili yao kutelekezwa ndani ya nyumba waliokuwa wakiishi huko katika Kijiji cha Mkolye Wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa waTabora, ACP SAFIA JONGO amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa moja usiku ikiwa ni mfululizo wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatia ambayo yameendelea kutokea wiki hii huko mkoani Tabora.
 
Binaadamu ni hatari kuliko Simba na hawaogopi jela
 
Marehemu wapumzike kwa amani...pole kwa familia yak pia....

Mwanaume sijui alikumbwa na nn jamani
 
Ukimuuliza atakwambia wivu wa kimapenzi. Atakwambia alisalitiwa.

Ni mwanaume mpumbavu tu anaweza kuua mke ama mwanamke kwa sababu ya usaliti.

Na kosa kubwa linalopelekea matukio kama haya kutokea ni kua na mwanamke mmoja na ukampenda, hii kwa mwanaume ni sawa na kujaribu kumeza sumu ukiamini kwamba haitakuua, itakuua tu.

Wanaume wengi wanaojiua ama kufanya matukio ya kipumbavu kama haya makosa yao hua ndio hayo, kua na mwanamke mmoja na ukampenda na kumuamini 100%. Ipo siku usipoua basi utajiua ama utapata msongo mkubwa sana wa kimawazo.
 
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za mauaji ya mkewe na watoto wawili wanaodaiwa kuuawa kwa kupigwa kichwani na mchi wa kutwangia kisha miili yao kutelekezwa ndani ya nyumba waliokuwa wakiishi huko katika Kijiji cha Mkolye Wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa waTabora, ACP SAFIA JONGO amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa moja usiku ikiwa ni mfululizo wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatia ambayo yameendelea kutokea wiki hii huko mkoani Tabora.
Domestic violence mbaya sana na victims wahanga wengi ni wanawake
 
kuna watu bado hawajaevolve kufikia stage ya kuwa binadamu hivyo kuua ni kawaida hawana tofauti na wanyama.
Mkuu wanasaikolojia wanakuambia the strongest are the ones who can control their emotions.

Sasa hivi matukio ya domestic violence murder, murder suicide na homicides ni mengi sana duniani hata kwenye nchi tajiri. Na victims wahanga wengi ni wanawake.

Ni kumuomba Mungu tu akuepushe kwasababu hao wanaoua wanajikuta tu kwenye mazingira flani hivi halafu shetani hapo hapo anachukua advange.

Mimi nilivykuwa na ex wangu kila akianzisha chokochoko faster natoka zangu nje nakuwasha mjani nakupiga misele.
 
Haya matukio ya hovyo huwezi kuyasikia mkoani kwetu Lindi.
Kuna mikoa ina watu wenye roho za kishenzi sana
Lindi ni mkoa wa ukanda wa Pwani; ni miongoni mwa mikoa ambayo imeinteract na wageni wa kila kabla, wakati wa ukolon na hata baada ya ukoloni; ni watu wastaarabu na wala siyo WASHAMBA WA MAMBO YA MAPENZI

Ila hawa wa mikoa ya bara na kanda ya ziwa; wanacomplicate sana mambo ya mapenzi😁😁😁😁😁.

mwanamke kama unaona umemshindwa mwache fanya yako
 
Haya maeneo yetu haya yana ukatili sana wa kifamilia! Tabora, Shinyanga, Mwanza, hadi Geita na Kagera sio shwari sana mambo ya kifamilia. Idara ya Ustawi wa Jamii na wadau wengine watupie jicho la kipekee maeneo hayo!
 
Lindi ni mkoa wa ukanda wa Pwani; ni miongoni mwa mikoa ambayo imeinteract na wageni wa kila kabla, wakati wa ukolon na hata baada ya ukoloni; ni watu wastaarabu na wala siyo WASHAMBA WA MAMBO YA MAPENZI

Ila hawa wa mikoa ya bara na kanda ya ziwa; wanacomplicate sana mambo ya mapenzi😁😁😁😁😁.

mwanamke kama unaona umemshindwa mwache fanya yako
... watu wasiotahiriwa mwili na roho ni shida.
 
Back
Top Bottom