Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Usongo ,Nkinga wilayani Igunga anayefahamika kwa jina la Thadeo Shahibu amepandishwa kizimbani hii leo katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya kukutwa anamiliki mnyama Kakakuona kinyume cha Sheria namba tano ya uhifadhi Wanyapori ya mwaka 2009 ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya Dola la Kimarekani 960 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 2.2 fedha za kitanzania.
Akiwa ameambatana na Mnyama huyo kakakuona,Thadeo Shahibu amefikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora,Mbele ya hakimu Chiganga Tengwa akikabiliwa na shitaka la uhujumu uchumi baada ya kukutwa na Mnyama huyo nyara ya Serikali.
Umati wa watu waliofika mahakamani hapa wakiwemo watumishi wa mahakama walionekana kushangazwa na mnyama huyo ambaye wengi humtafsiri kama ni mnyama wa bahati kumuona hasa katika mazingira ya mjini.
Mtuhumiwa Thadeo Shahibu alikamatwa akiwa na mnyama huyo katika kijiji Cha Ziba wilayani Igunga wakati akiwa kwenye harakati za kumuuza akidaiwa kumtoa huko Mtera mkoani Iringa ambaye alisafirishwa kwa Pikipiki
Kwa mujibu wa maelezo ya Wakili upande wa Jamhuri Tito Mwakalinga,mtuhumiwa Thadeo Shahibu mnamo tarehe 15 Julai mwaka huu majira ya usiku alikutwa na mnyama huyo kinyume na kifungu cha 86 kidogo cha kwanza na cha pili cha sheria namba 5 ya uhifadhi wanyamapori.
Hata hivyo kutokana na uzito wa shauri hilo la uhujumu uchumi namba 45 la mwaka 2019,mahakama hii ya hakimu mkazi imelazimika kumsomea shitaka mtuhumiwa na hakutakiwa kujibu chochote kwakuwa mahakama hiyo haina nguvu ya kisheria ya kusikiliza shauri hilo hivyo kesi hiyo itatajwa tena August Mosi mwaka huu huku mahakama ikimpa nafasi mtuhumiwa ya kuomba dhamana,wadhamini wawili shilingi million 5,sharti ambalo hakuweza kulitimiza na hivyo kupelekwa Gereza la mahabusu.