Tabora: Amuua mke wake kwa kisu kisha ajiua kwa kunywa sumu. Aacha Ujumbe

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Mwanaume mmoja wilayani URAMBO Mkoani Tabora amemuua mke wake kwa kumchoma visu na kisha kujiua kwa kunywa sumu na kuacha ujumbe wa barua kwa familia ya mke wake. "Nilimuoa siku moja na tutakufa siku moja, mtuzike pamoja".

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji cha Maswanya Songa Juma amemtaja mwanamke aliyeuwawa kuwa ni Mariam Nassoro ambaye ameuwawa na mume wake aliyefahamika kwa jina la Issah Seleman.

Chanzo: CG FM Tabora
 
Hizi habari wala hata sio ngeni ni vile tu siku hizi kumekuwa na urahisi wa habari kupatikana mtandaoni na kuenea kwa uharaka zaidi.

Ila inasikitisha sana kukatisha maisha ya mwenzako kisa kufata hisia zako tu
 
Kuna watu wanastahili kutozikwa....maybe hilo likianza wafanyika watapata akili....kuwe tu jalala la kutupa miili ya watu wanaofanya mauaji kama haya.
 
Mwanaume mmoja wilayani URAMBO Mkoani Tabora amemchoma visu mke wake na kisha kujiua kwa kunywa sumu na kuacha ujumbe wa barua kwa familia ya mke wake. "Nilimuoa siku moja na tutakufa siku moja ,mtuzike pamoja"

Marehemu huyo aliyefahamika kwa jina la ISSAH SELEMANI amemchoma kisu aliyekuwa mke wake Mariam Nasoro ambapo Mwenyekiti wa kitongoji cha MASWANYA Songa Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Chanzo: CG FM Tabora
Mwanaume amejiua kwa kunywa sumu.Kuhusu mke hujaeleza kuwa alivyochomwa visu alikufa au alinusurika.
 
Aisee saa zingine hawa wanawake wawe wanasoma upepo na kurudi kwao.
Bora akajiuze kuliko kuuliwa

Naumia kusikia mtu kamuua mtu kwa sababu ya mapenzi

Sio mapenzi,wanawake wengi husingizia watoto.Hivyo watoto ndio husababisha vifo vya wanawake.

Maranyingi Kama mwanamke hujazaanae mkizinguana nirahisi kuondoka zake.
 
penzi tamuu la umpendaeee... halafu eti unakuja kufahamu jamaa wanakumegeaaa DUHHH astakhaga;oah;ab
 
Sio mapenzi,wanawake wengi husingizia watoto.Hivyo watoto ndio husababisha vifo vya wanawake.

Maranyingi Kama mwanamke hujazaanae mkizinguana nirahisi kuondoka zake.
Hapana sio watoto bwana. Hawa wanashindwa kuondokankwa sababu ya kupenda kuhudumiwa tuu. Mwanamke ambae anajimidi finacially ataondokanfasta tuu na anabeba na watoto wake. Ma superwoman ni wachache sana, wengi ni wannawake tegemezi
 
Back
Top Bottom