TABOA: Stendi za mabasi ya mkoa na daladala wawepo wasafiri pekee wafanyabiashara waondolewe kupunguza msongamano

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Katibu mkuu wa chama cha wasafirishaji abiria (Taboa) ndugu Mrutu ameiomba Tamisemi kuhakikisha vituoni wanabakia wasafiri tu ili kupunguza msongamano nyakati hizi za majanga ya Corona.

Mrutu amesema hata kwenye vituo vya daladala mfano Makumbusho kuna msongamano mkubwa sana wa watu lakini wengi wao siyo wasafiri. Hivyo ni muhimu wakabaki abiria wanaosubiri usafiri.

Source ITV
 
Hili wazo niliwahi kuliwaza Siku nyingi sana kwanza Abilia anajua atapanda basi gani? Hii mambo imesababisha nauli kuongezeka bila sababu
 
hilo eneo JPM hajaligusa na anaweza asiliguse kabisa kwa sababu, tokea mwanzo alitamkaa wamachinga wasibughudhiwe si rahisi kuyaedit maamuzi yake na ukiwazuia itakuwa ni vita isiyo na mwamuzi, labda ianzie sasa hivi kwa sababu za covid19 na zianzie hapo kuwekewa mwongozo,
 
Mzee Mrutu umenena vyema kabisa, lakini sidhani kama wahusika wataamka ktk usingizi wa pono kutekekeleza hili. Tena wao ndio walitakiwa walione hili mapema sijui wanamsubiri Raisi aseme!
 
Ni hatua njema lakini kwa bahati mbaya haitoshi.

Huu ugonjwa bado hatujauelewa sawa sawa. Inahitaji mgonjwa mmoja tu kuambukiza maelfu kwa muda mfupi tu.

Angel Merkel alisema haijakuwapo changamoto kama ya ugonjwa huu tokea vita vikuu vya pili vya dunia.

Huu ugonjwa unataka ufumbuzi kamili si nusu nusu (total not a partial solution).
 
Yale mabasi ya kampuni ya kirumo,yanayomilikiwa na Ainea mrutu yapogo au amekuwa amebakia kuwa msemaji wa Taboa kulamba hela ya chama? Taboa pitieni katiba yenu upya mpate kiongozi mwingine anayemiliki mabasi jamaa kampuni yake ilishakufaga huo.
 
Yale mabasi ya kampuni ya kirumo,yanayomilikiwa na Ainea mrutu yapogo au amekuwa amebakia kuwa msemaji wa Taboa kulamba hela ya chama? Taboa pitieni katiba yenu upya mpate kiongozi mwingine anayemiliki mabasi jamaa kampuni yake ilishakufaga huo
Umeuliza swali na kujijibu bwashee!
 
Yale mabasi ya kampuni ya kirumo,yanayomilikiwa na Ainea mrutu yapogo au amekuwa amebakia kuwa msemaji wa Taboa kulamba hela ya chama? Taboa pitieni katiba yenu upya mpate kiongozi mwingine anayemiliki mabasi jamaa kampuni yake ilishakufaga huo
Binadamu wengine wana chuki binafsi na wivu sana. Yaani issue inahusu msongamano stand za magari, badala yakujadili mada wewe unaleta mambo mengine. Ungeianzishia Thread yake ungeeleweka vizuri.
 
Binadamu wengine wana chuki binafsi na wivu sana. Yaani issue inahusu msongamano stand za magari, badala yakujadili mada wewe unaleta mambo mengine. Ungeianzishia Thread yake ungeeleweka vizuri.
Hoja ya msingi ni Taboa na corona.ila la kirumo liko pale pale.
 
Back
Top Bottom