Tabia zipi huzipendi kwa ndugu yako, mpenzi wako, rafiki yako au hata mzazi wako?

Hii ya kutokuaga si ya kwako tu, hata mimi ninayo sana hii tabia, tena mimi hata text situmi ni nasepa tu mazima naendelea na mapambano ya kimaisha
Kwa kweli kuaga ni kipaji,
Nasemwa sana nibadilike ndio nikijitahidi natuma text.

Uko poa lakini?
 
Aah ukimtembelea Bi mkubwa we jiandae kwa hilo yaan unakuta mtu humjui ila anapewa full CV yako, ukilalamika anakwambia c best yangu😂. Achilia mbali kuambiwa twende tukasali kanisani kwetu...kumbe shida sio kusali bali zoezi lake la utambulisho baada ya misa lifanyike. Lazima utaomba pooh😩
Ahhahaha wengine watafatwa hata kama umelala utaamshwa yaan majiran wanafatwa mtoto wangu amekuja 😂😂😂😂
 
Nachukia wanaopenda kuongelea maendeleo yao yaan anajua kabisa bado unapambana ila sasa ukikaa nae mara oh unajua gari yangu juz alizingua mara sijui nyumba angu ya kimara INA ufa nimesahau kumpigia fundi mara oh duka langu Leo sijafungua kijana kaniibia

Yaan wana misifa marafiki wa hivi akienda chooni akatoka utasikia dah best nilijisahau nikaanza kutafuta nibonye wapi niflash kumbe sipo kwangu
 
Sipendi kelele iwe kutoka kwa Mama/ndugu

Sipendi kuambiwa nini cha Kufanya Katika maisha yangu

Sipendi tabia ya Dada angu fulani akikufanyia kitu mpaka atangaze..yani ana ile bila mimi kitu fulani kisingefanyika..bila Mimi fulani asingekuwa hivi.😏

Sipendi tabia ya marafiki wanaoniongelea vibaya iwe kwa mpenzi au watu wa karibu

Sipendi tabia za marafiki wanaojifanya wanamjua sana mwanaume wangu na kujichekesha chekesha ovyo..mfyuuuuu
Hiyo ya mwisho ndiyo hofu yako...




Cc: mahondaw
 
Mpenzi wangu anatabia mbaya zifuatazo
1. hamuheshimu kabisa mama yangu mzazi aliwahi kumkatalia mara kadhaa kutumwa....
2. nikiwa sina pesa huwa ananinunia
3. hajui kutumia lugha ya kushawishi kuniomba jambo.

tabia zote hizo nimeaamua kuzivumilia kwasababu tu nimezaa nae na sipendi mtoto wangu aje kunilaumu kwa kukosa malezi ya baba na mama...ila kiukweli kabisa ndugu msomaji nilisha jiwekea kuwa mtu akinizaraulia mama yangu hanifai...
tatizo ni mtoto tu ila dalili zote zinaonesha hapa sijapata ila nimepatikana...TIME WILL ANSWER
 
Mdogo wako HUMKOPESHI unampa tu ndiyo raha ya kuwa mkubwa. Si ungeukataa ukubwa ili uwe kitinda mimba? 🙊🙊🙊
Mdogo wangu kunikopa hela halafu harudishi. Na cha ajabu akiniomba tena huku bado namdai basi ataniahidi ahadi zake hewa zenye ushawishi ambapo huwa nashindwa kabisa kumyima aisee.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom