101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,117
Habari wakuu,
Mimi kama Kijana wa kitanzania nina mengi ya kusema kuhusu familia zetu.
Wengi wetu katika familia hizi zetu za kiafrica tumekuwa wahanga wa mahaba ya wazazi kuelemea upande mmoja Kwa Baadhi ya Ndugu zetu.
Wazazi wengi wameshindwa kubalance mahaba kwa watoto ndani ya familia na kupelekea Ndugu wa familia moja kufarakana na kugombana.
Wazazi wengi wamekuwa hawaamini kama kweli wanamahaba kwa mtoto wao fulani ila hili hujitokeza pindi anapofanya makosa
1. Huwa hawaamini kama kweli kafanya hilo kosa
2. Wanaona hamumpendi
3. Mnamuonea
4. Hamjampa nafasi
Ikitokea hajafanikiwa kimaisha yule kipenzi chao basi utasikia
1. Hamumpendi Ndugu yenu
2. Mnamroga
3. Mmemtenga
4. Mimi nikifa mtamuua
5. Hata kama anamakosa ndio Ndugu yenu
Wazee wetu wakiwa watu wazima na wamezeeka hata uwafanyie jambo kubwa kiasi gani hawahisi kama umefanya chochote, lakini Yule kipenzi chao akiwapa hela hata Elfu 5 au kuja kuwaona atahadithia siku nzima.
Jambo hili la mahaba ya wazazi kuelemea upande mmoja limeperekea kuharibu umoja wa familia nyingi
Wito wangu kwa vijana wenzangu.
Sisi ni wazazi mda si mrefu tutakuwa na familia zetu na wengine tunafamilia tayari tujitahidi kuzijenga familia zetu katika upendo Sawa Kwa wote tufiche mahaba yetu kwa mtoto mmoja ili kujenga familia imara.
Karibuni tumwage shuhuda zetu.
Asanteni