Tabia za Watoto kufanyiana ukatili inakua, Watanzania wenzangu tuamke, nani wa kulaumiwa hapa

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
420
1,047
Inawezekana hii haizungumzwi sana katika vyombo vya habari kwa kuwa wanahabari wengi wanatazama kinyume chake lakini ukweli ni kuwa kuna tatizo limekuwa likiibuka la watoto kufanyiana ukatili wao kwa wao.

Tunajua kuwa asilimia kubwa ukatili kwa asilimia kubwa umekuwa ukifanywa na watu wazima dhidi ya watoto lakini ikitokea umefanywa na watoto kwa watoto mara nyingi inaonekana siyo habari.

Ukweli ni kuwa mitaani huko kuna kesi nyingi za watoto kufanyiakana ubaya wao kwa wao, Serikali imekuwa kimya kuelezea hilo au mamlaka zimekuwa na ‘ububu’ flani kutotaka kuieleza jamii juu ya tatizo linalotukabili.

Wikiendi hii iliyopita nilianza kumsikia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima akigusia suala hilo na binafsi nampongeza.

Jamani wazazi na walezi tuamke na tushirikiane na taasisi zinazowalea watoto hasa shule katika ku monitor tabia za watoto wetu.

Nimemsikia Waziri Gwajima akieleza kusikitishwa na tabia ya baadhi ya wanafunzi kufanyiana ukatili mashuleni.

Gwajima alizungumzia matukio hayo juzi Mkoani Shinyanga, wakati akipokea taarifa ya uzinduzi wa Programu ya malezi na makuzi bora ya mtoto kwa njia ya mtandao, kutoka Shirika la ICS ambalo linajihusisha na shughuli za utetezi wa haki za watoto na wanawake mkoani humo akasema, namnukuu:

"Nimekuwa nikipokea meseji nyingi sana kuhusu watoto kufanyiana ukatili wao wenyewe mashuleni, wakienda huko msalani wanafanyiana vitu vya ajabu," alisema Waziri Gwajima.

"Naagiza maofisa ustawi wa jamii toeni elimu mashuleni kwa kushirikiana na walimu ya kupinga ezoea kusikia watu wazima wakiwafanyiaukatili watoto, lakini sasa hivi wameanza kufanyiana ukatili wao wenyewe sijui tunaelekea wapi,"

Hivyo, Watanzania tuamke na tuhakikishe na kuchukua hatua mapema.

Nani ambaye mtaani kwake kuna matukio ya ajabu ajabu ya ukatili ya watoto kwa watoto?
 
Vipi huo muda wa kulea hao watoto tunaupata wapi... Wakati serikali imewachukua shuleni muda mrefu siku nzima mpaka weekend mpaka likizo...

Toeni huo mfumo mbovu wa elimu... Wasome kidogo warudi nyumbani wafunzwe na ulimwengu...
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!
Umelidekeza toto toka linazaliwa,
Jirani akilifinya kidogo kelele mpaka mtaa wa pili!
Toto linaachiwa kutazama ponografia kutwa nzima!
Ole wenu wazazi hizo shule za bweni, maadili yebadilika sana!!
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!
Umelidekeza toto toka linazaliwa,
Jirani akilifinya kidogo kelele mpaka mtaa wa pili!
Toto linaachiwa kutazama ponografia kutwa nzima!
Ole wenu wazazi hizo shule za bweni, maadili yebadilika sana!!
Ndio umeandika nini hapa? sababu hakieleweki.
Point yako iko wapi?
 
ni muda muafaka kuwafunza wanetu kung-fu ili wajilinde wenyewe

#niguse ninuke
 
Back
Top Bottom