Tabia za wanyama walizanazo watu zenye kuweza kuua Taasisi au Kampuni au Ofisi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,850
928


Tabia za wanyama walizanazo watu zenye kuweza kuua Taasisi au Kampuni au Ofisi.

Bata:
Kujivutavuta, hufanya kazi polepole na kuendekeza uvivu mpaka mambo ya kikundi yanazorota au kufa kabisa.

Bundi:
Mtu anayefikiria ana akili kuliko wote kwenye kikundi- hutumia lugha ngumu na haeleweki

Chura:
Hurudiarudia kitu kile kile mpaka anawachosha wenzake kundini

Kenge:
Hatumii akili sawasawa, ujinga mwingi na hufanya maamuzi ya ovyo yenye kuwakatisha tamaa wenzake

Kiboko:
Hulala lala na kupiga miayo. Wakati wenzake wanachacharika yeye ni kukaa tu, hafanyi kazi.

Kifaru:
Yeye hushambulia wengine kwenye kikundi bila sababu

Kinyonga:
Kigeugeu, akiwa kwa mwanakikundi huyu anasema hili na akiwa kwa mwingine anasema tofauti

Kobe:
Hujitoa akiudhiwa, hana uvumilivu kwenye changamoto zinazokabili kikundi.

Kuku:
Kuvuruga palipotengenezwa, huenda tofauti na maono ya kikundi kwa kujali na kuzingatia mambo ya muda mfupi tu.

Mbuni:
Huficha kichwa na hufikiri hakuna shida kwenye kikundi hata kama zipo shida nyingi

Nyati:
Kujihami tu kwa sababu ya woga. Hakosolewi, ukimgusa tu anaazisha vita vya maneno au kupigana

Nyoka:
Anajificha huku akiuma bila kusema. Mchonganishi

Nyumbu:
Mwoga na hatumii akili kabisa.

Paka:
Yeye hutaka ahurumiwe tu na wenzake, hana mchango wowote kwenye kikundi.

Panya:
Hachangii chochote yeye hujificha tu na kujitokeza wakati wa neema.

Popo:
Hana msimamo. Kwa wanaokubali hoja yupo na kwa wanaopinga hoja yupo! Haeleweki.

Punda:
Mgumu kubadilika. Hata umuelimishe vipi, misimamo yake ni ile ile ya zamani.

Samaki:
Hachangii hoja, kazi tu, kukwepa na kutoweka na huonekana hali ikitulia na kuwa shwari.

Simba:
Hupigana kama mawazo yake hakubaliwi na wanakikundi wengine.

Sungura:
Hukimbia kama kuna dalili za hatari na kwenda kinyume na makubaliano ya kikundi

Tausi:
Yeye huringa kwa mambo mazuri aliyonayo ambayo wanakikundi wenzake hawana.

Tembo:
Hufunga njia bila sababu watu wasipite. Huzuia mawazo na maamuzi ya kikundi yasifanikiwe bila sababu.

Tumbili:
Mizaha mizaha tu wakati wote hayuko makini hata kwa mambo muhimu ya kikundi.


KILA MDAU AJITAFAKARI INAWEZEKANA KUNA MAHALI AMEGUSWA.
 
Back
Top Bottom