Tabia za mjamzito za hasira na kususa huanza muda gani?

Kindeena

JF-Expert Member
Sep 27, 2017
9,014
15,695
p.jpeg

Nina mpenzi ambaye tumedumu miezi kadhaa sasa mabadiliko yake ndiyo yamenifanya niombe ushauri hapa mwezi wa kumi mwaka huu tulipanga tutafute mtoto, ambapo tulijamiana sasa kabla haijapita wiki na nusu, akaanza tabia ambazo hakuwa nazo mwanzo.

Mfano, alianza kuniambia mapenzi ya kupigiana simu kila wakati hayawezi, amezoea kuwa huru na kwamba yeye ameathirika kisaikolojia na mapenzi hayamuendeshi kivile mimi nikamjibu, "baby sasa nikikumiss nisikutafute"? Akasema siyo kila wakati simu nikamwambia kwa siku nikupigie mara ngapi?Akajibu "utajua mwenyewe" nikamuuliza mbona una hasira na umebadilika ghafla hivii.

Maana mwanzoni alikuwa anajibimu meseji na simu anapokea hata kama yupo ofisini maana kaajiriwa taasisi fulani ya fedha.

Nikimwambia "baby nakupenda" anajibu "haya". Nikimuuliza unanipenda? Anakaa kimya, baadaye anauliza kwani vipi?

Sasa juzi tarehe 16 mwezi huu kaniambia amepima akakuta ana mimba yangu kipimo kanunua dukani mimi nimefurahi maana ninapenda sana watoto aliniambia kuwa alihisi mabadiliko ya mwili ndiyo akaenda kupima.

Pia akaniambia niende kujitambulisha kwao kabla mimba haijawa kubwa, nikamwambia sawa, asiwe na shaka.

Sasa swali langu waungwana lipo hapa, kwamba je, mwanamke akishika mimba tabia yake huanza kubadilika baada ya umri gani wa mimba? Ninauliza hivi, maana huyu mpenzi wangu kapunguza kuwa romantic chini ya wiki moja na nusu hivi toka nijamiane naye.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom