dr Akanyonyi Ako
JF-Expert Member
- Dec 31, 2012
- 244
- 86
Katika pitapita yangu, nimekutana na wateja wa Benki moja hapa Geita, wakilalamikia tabia ya Mameneja wa matawi ya benki hiyo mawilayani kuomba ten pasenti pale wanapopata mikopo.
Yaani; ni hivi ukiomba mkopo wa milioni 3, hatua za kupitisha zikafanikiwa, meneja anakupigia simu ikiwa ni pamoja na kutuma meseji za kuomba umpatie teni parcenti. Baada ya zoezi la asilimia kutolewa wateja hawa huwa wasumbufu kurejesha mikopo na hivyo kupelekea usumbufu kwa maafisa mikopo na wale wanao fuatilia marejesho katika matawi husika.
Nimeongea na walau maafisa mikopo watatu toka matawi matatu tofauti nao wamekili kuwapo kwa tatizo hili; Aidha baadhi ya wateja yaani wawili walikili kushawishiwa ama kutakiwa kutoa teni pasenti pale walipo pata mikopo.
Je wadau mmeishakumbana na tatizo hili? Walioko kanda ya ziwa hasa Geita wanaweza kusema.