Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
(1) Unakuta mtu anaongea kwa simu kwa kupaza sauti hadi inakuwa kero kwa wengine. Sijui unataka uonekane mtu wa mipango au ndo vipi? Eti unajua kwenye ile indavyuu mimi pekee ndo nilifanya vizuri. mmxxsh hiyo intavyuu yako sisi inatuhusu nini.

(2) Gari ina AC wenzio wooooote wamefunga vioo wanakula unyunyu wewe umeacha madirisha wazi ukidai eti hupendi AC, mbona gari zisizo na AC ni nyingi kwanini usingeenda kupanda hayo?

(3) Umewekewa video au redio kwa sauti ya wastani kuruhusu hali ya utulivu ndani ya gari. Wewe unapaaza sauti kwa konda eti sauti ni ndogo iongezwe. Sio kila mtu anapenda sauti ya juu achilia mbali hiyo video au redio unayosikiliza.

(4) Kwenye hizi video hasa za action au vichekesho. Wewe unapatwa na mdadi unaanza kurukaruka au kuchekacheka hovyohovyo tena kishabiki utafikiri mwehu. Sio kila mtu anapenda makelele.

(5) Unalala kwenye siti yako hadi unakoroma kama nyau wa mwituni. Kibaya zaidi unamuegemea mtu wa siti ya jirani na kumwagia maudenda yako.

(6) Muda wote wewe unachezeachezea simu yako wakati unajua huna chaja. Matokeo yake unaanza kugongea chaja ya simu kwa wasafiri wengine.

Ukijiona unafanya hayo kuanzia sasa ujijue wewe ni mshamba na unakera wengine, jirekebishe.
 
Hahahaha eti "indavyuuu".

Ila mimi hii tabia ya kuwekewa mifilamu mara manyimbo safarini inakera sana maana nyingi video hazina maadili kabisa na safarini mnakuwa watu mbalimbali inakuwa sio poa. Watu wawe wabunifu sio minyimbo ya kibongo maudhui za ngono tu mwanzo wa safari hadi mwisho.
 
Bila kusahau wale kina mama wanaosafiri na watoto wawili huku wamekata seat moja

Nilishawahi kujikuta dada msaidizi wa mtoto mwanzo hadi mwisho wa safari, yaaani kale kadogo nimekashikilia mimi, kale kengine kadada mtu kameshikwa na mama yake

Mbaya zaidi kale katoto kalinipenda na kunizoea mapema sana, kila muda dada hivi dada vile mara kanilishe vitu kanavyopewa na mama yake

Sio kwa ubaya, lakini ni usumbufu... kama una watoto wadogo wawili jitahidi kuweka seat mbili aseee

Siku hizi namuagiza anayenikatia ticket ahakikishe nakaa na mkaka
 
Kuna wale matumbo mpakile, yakipita mahindi ya kuchoma twende, ya kuchemsha twende, mayai twende, sijui biscuit mpaka inakua kero though pesa ni zao.


Let's meet at the top, cheers 🍻

Ila Huwa wana roho nzuri ya kugawa vitu vyao, Kuna mmoja alinikaribisha ndizi za kukaangwa na kuku af asubuhi tu, kila centre kubwa tukifika ananunua kitu cha kutafuna iwe mayai, matunda hadi mahindi.

Tulipofika kituo cha kupata lunch naye akashuka kula ubwabwa na kuku. Nilishangaa kimoyomoyo ila sikumind
 
Watu wanakula hadi miwa too little
Hahaha! Umenikumbusha beki tatu mmoja nilikjwa natoka Mtwara sasa ile asubuhi gari ikasimama maeneo ya Mnazi Mmoja Lindi kama saa tatu asubuhi hivi, sasa yule beki 3 akanunua miwa ya 1000 ambayo haijamenywa, nilidhanilabda ni zawadi huko aendako,

doooh akaanza kuimenya na meno na kuanza kuila hehehe! Akajaza dust bin ya gari na makapi ya miwa na hakuchukua round akaanza kutapika juice ya miwa alitapika sana vitenge vyake vyote vililowa matapishi hadi vingine ilibidi gari isimame achukue bag kwenye buti ili atoe vitenge vya ziada.
 
Back
Top Bottom