Tabia za jamii kikanda zina athari kiasi gani kwa taifa?

kamjabari

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
1,132
1,640
Nimekuwa nawasikia watu wengi wakisema viongozi wa ju wa nchi (Rais) wanavyo ongoza nchi huathiliwa na ukanda wao, wengi wakaenda mbali kwamba Pwani na Bala Kuna haina za kiuongozi zisizo fanana kimtazamo hata kama wana tawala nchi kupitia chama hicho hicho.

Viongozi (rais )wa bala wanapo pewa dhamana ya kutuongoza hujikia sana kujenga misingi ya kiuchumi kwa weledi na kusimamia kwa uthabiti mkubwa, lakini udhaifu wao huwa ni kuto zingatia sana Uhuru wa watu na Demokrasia.

Viongozi (rais) wa Pwani wao hujikita zaidi kuwezesha watu wao kuwa huru na kuendesha nchi kwa misingi hiyo, pia udhaifu wao ni kushinwda kusimamia miundombinu kwa kwa uthabiti wakutosha.

Mfano Mwalimu Nyerere, Mkapa, Magufuli walibana sana kwenye uchumi wa watu mmoja mmoja na kujitahidi sana kujenga miundombinu endelevu na kuweka nchi katika matumaini mapya ya maendeleo ya nchi baadaye!

Lakini Demokrasia haikuzingatiwa kwa kiasi cha kutosha.

Mwinyi, Kikwete tawala zao zilifurika pesa mfukoni mwa watu hasa walikuwa na mirija mingi ya kunyonyea.

Lakini usalama na maendeleo ya nchi vili teteleka hasa miundombinu Kama Umeme, Afya, Elimu, nk Ilikuwa ni tabu kubwa.

Karibu tujadili kwa kina nini kifanyike ili kuwe na uiano sawawa tawala hizi.
 
Back
Top Bottom