Tabia za baadhi ya viongozi wetu wa Serikali zinaakisi tabia za baadhi ya wakuu wa shule nchini

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,127
Huwa mara nyingi zinapotajwa sababu za elimu yetu kuwa na utapia mlo unaopelekea kudumaa tabia ya baadhi ya wakuu wa shule kuchangia hali hiyo huwa haielezwi sana pengine ni kwa sababu haifanyiwi utafiti wa kutosha, kwa walimu hili wanalielewa vizuri sana na kwa wadau wa elimu pia wanaju hilo.

Hakika tabia za badhi ya viongozi wa kisiasa na kiserikali waliokuwa walimu ndiyo hali halisi ya baadhi ya wakuu wa shule kwa walimu walio chini yao, ukimuona mwl. nchi hii muinee huruma baadhi ya changamoto zake hazisemi, je baadhi ya tabia hizo ni zipi?

1. Ubabe, kuna wakuu wa shule hadi walimu wenzake wanahesabu kila kukicha miaka yake ya kustaafu, yaani anachotaka yeye ndo hicho tu hakuna wa kupinga, akiona yupo anaye mkosoa hapo visa, uhamisho hakuna kupendekezwa kwenye shughuli maalumu, yaani kiufupi atataka akuonyeshe yeye ni nani?

2. Ubinafsi na roho mbaya, hawa watu kiufupi shule waliona kama assets zao, hapa Magufuli kawanyoosha kidogo kwa kutoa michango, yaani mkuu wa shule unakuta anakuwa mbinafsi hata kwa vitu ambavyo ni haki ya mwl yeye ataibana tu ili mradi apigiwe magoti, du hata kumpa nyumba ya shule akaishi lazima angalie nani anamsujudu.
Maslahi yao kwanza yaani kama wewe unaonekana kuhoji hoji basi baadhi ya vitu utavisikia kwa mbali kama ubunge wa bunge la Afrika mashariki. Yaani hata barua ya kwenda kusoma kupitishia hadi sijui akamuulize mke wake?

3. Dharau, majivuno na udhalilishaji.
Kuwadhalilisha walimu wa chini yao hawajambo tena hata mbele ya wanafunzi, na kigezo kikubwa kujifanya wao wanauzoefu wa muda mrefu hivyo hawawezi kushauliana na vijana.
Huwa hawajali utu wa wenzao wao madaraka ndo muhimu zaidi.
Hizo ni baadhi ya tabia za wakuu wa shule kwa walimu wenzao na tabia hizo baadhi yao huzibeba hata wanapopata madaraka makubwa.

NB. Sio wakuu wote wa shule wapo hivyo wengine ni viongozi wazuri tu, na wenye tabia hizo Mara nyingi ni wale wa 1980s.
 
Back
Top Bottom