Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,669
- 40,917
Habari wadau wa MMU,
Leo nimeona nilete hili jambo kwenu wataalam wa maswala ya mahusiano, hii ni baada ya tukio la siku chache zilizopita, ambapo nilikutana na vijana wawili waliopo katika mahusiano yao ambao kwa mtazamo wa haraka wanaelekea kufunga ndoa.
Kijana namfahamu na binti pia namfahamu kuliko ninavyomfahamu kijana, kilichonifanya nijiulize hili swala, ni kutokana na tabia za awali za huyu binti, ambazo kwa kweli zilikuwa si njema, katika jamii aliyokuwa akiishi yule binti hakuwa na sifa nzuri kwani hakuwa na tabia njema kwa wazazi na pia alikuwa ni mtu wa kuwa na mahusiano mengi mpaka kufikia hatua ya kuzushiwa mambo mengi mno, na kwa kipindi hicho alikuwa bado na umri mdogo tu.
Kwa jinsi ninavyomfahamu kijana nilitegemea kabisa kuwa alistahili kufanya due diligence kabla ya kujihusisha na binti, lakini naona maamuzi yake yatakuwa yamefunikwa na mahaba, kwani hata hivyo kwa historia ya huyo binti sio ajabu kabisa namna alivyofanikiwa kuishi maisha ya sasa.
Ingawa kwa kuangalia kwa haraka utaona kama binti kabadilika ( kaokoka) lakini bado na mashaka kama mabadiliko hayo ni ya kudumu, na huo ndio msingi wa bandiko kama ni kwa namna gani tabia za awali zinaweza kuathiri mahusiano mapya?
Je mtu anaweza kabisa kubadili tabia na kuwa mpya??
Baada ya kuona wanandoa hao watarajiwa nikafikia hitimisho lifuatalo;
1. Ni muhimu mno kwa vijana kuchunguzana kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kudumu. ( Ni muhimu sana).
2. Ni muhimu kwa vijana kuwa makini na matendo yao wakati wa ujana, kwani huko mbeleni matendo hayo huibuka na kutufuatilia, hata na kutaka kuharibu furaha tutakazokuwa nazo kwa wakati huo.
3. Ni muhimu mno kumshirikisha Mungu katika kila jambo na hasa hili la kupata mwenza kwani kuna watu ni mabingwa wa deception.
Karibuni wadau.