Kategele
JF-Expert Member
- Oct 7, 2017
- 968
- 2,230
Kama kawaida baada ya kumaliza chuo nikaingia mtaani kusota na maisha bahati nzuri nikapata intern kwenye moja ya taasisi za serikali zinazolipa vizuri.
Changamoto ikawa kumbe kwenye taasisi hizi za serikali inatakiwa ufanye kazi kwa bidii bila kusahau kujipendekeza kwa boss.
Kwa jinsi nilivyo tabia yangu ya kutopenda kujipendekeza wala kufitini wafanyakazi wenzagu mimi nikawa natimiza Majukumu kama kawaida.
Kumbe ilitakiwa niwe naenda hata kumuona boss personly angalau mara moja kwa wiki kumsalimia tu ambavyo wengine hufanya sasa mimi nawaza nikamuone manager nimweleze nini cha zaidi wakati meeting za Kila wiki tunakutana na kila mtu anawasilisha ripoti yake?.
Basi bwana boss akaanza kulalamika ooh sina msaada kwenye office ikabidi nifuatilie kujua ninakwama wapi bassi wadau wakanitonya jipendekeze nenda hata mara moja peleka umbea wowote ule atakukubali tu.
Asikwambie mtu hakuna kazi ngumu Kama kuwa mmbeya eneo la kazi Kama hauna tabia hiyo.
Mimi nikasema potelea mbali ilimradi natimiza Majukumu yangu na nipo qualified siwezi kujipendekeza kwenye ofsi hii nitapata kazi hata kwingine.
Mkataba wa intern ukaisha boss Kama kawaida akaaniambia nitafute kazi sehemu nyingine.
Mwamba nikaona siyo kesi nikaingia mtaani nikapata kazi kampuni nyingine ya kibongo aisee kule ndio ikawa balaa bila kuwa mbeya humalizi mwezi unatimuliwa boss anataka kila siku mpishane na wafanyakazi ili apate taarifa mara huyu kapeleka fulani mwizi kaiba mafuta, kifusi.
Daah nikaona pia isiwe kesi nikaacha kazi.
Sasa Nina mwaka nasota mtaani nimezunguka kinoma hamna kazi kila Kona patupu wadau wanashauri tafuta hata viongozi wa kisiasa ujipendekeze kazi siku hizi kujuana mimi naona wananisumbua tu.
Natafuta kazi nikiamini qualifications zangu zitanibeba lakini patupu nimeapply sehemu nyingi hata kuitwa hakuna.
Nikatafuta mpaka sehemu za vibarua patupu. Sasa nawaza hii tabia ya kutojipendekeza nitaachaa vipi maana kubadili tabia ni ngumu kama kubadili ngozi.