Tabia yake hii inanitesa

smartmgabe

Member
Nov 15, 2013
25
6
MImi ni kijana wa umri wa kati , nimeoa miaka miwili iliyopita
katika maisha yangu mapya ndani ya taasis ya ndoa nimekumbana na changamoto
inayonitesa sana , mke wangu ana asili ya kumiliki kila kitu nikiwa na maana ya kupenda kuweka kila kitu chini ya utawala wake, inafikia hatua anataka anichagulie rafiki wa kuwa nae,
muda wa kutoka kazini bila kuzingatia majukumu niliyonayo?
tunapotoka nae hata ikiwa churchi ananichagulia upande wa kukaa

so kuna wakati naona naishi maisha ya mke wangu na sio maisha yangu in other way round i feel like a captive to her,
nachoomba hapa ndg zangu ni jinsi gani naweza deal na changamoto hii .
 
Kama hii stori ni ya kweli, basi wewe unamatatizo kumkichwa...I mean hauko sawa kichwani.

Anyway hayo ni maisha yenu na wakati mnatongozana hatukuwepo...ahsante napita zangu
 
Hukulijua hilo wakati mna-date????

Solution ni kusimama kama mwanaume kwenye ndoa, nyie si ndio vichwa??
 
Kama hii stori ni ya kweli, basi wewe unamatatizo kumkichwa...I mean hauko sawa kichwani.

Anyway hayo ni maisha yenu na wakati mnatongozana hatukuwepo...ahsante napita zangu

come on man! Nini maana ya jukwaa la mapenzi na urafiki?nini maana ya kuleta huu uzi?
Kwani hata ungekuwepo wakati wanatongozana ungeleta tofauti gani?
Stop being mean and negative dude! Life is too short to hate
 
mweleze kuwa hupendi. Na uact on what u want. Usimshirikishe mtu kwanza(marafiki,majirani,ndugu) kwani bado mapema sana. And despite,its something u can handle. Talk to her and Act on it,uwe na msimamo.
 
mweleze kuwa hupendi. Na uact on what u want. Usimshirikishe mtu kwanza baddo mapema sana. And despite,its something u can handle. Talk to her and Act on it,uwe na msimamo.

Haya Asimshirikishe mtu ila Aje Hapa Jamvini kwa kua kuna Mbuzi zitajibu tu, watu hawapo hapa.....
 
Haya Asimshirikishe mtu ila Aje Hapa Jamvini kwa kua kuna Mbuzi zitajibu tu, watu hawapo hapa.....

kwani we mbuzi? Namanisha marafiki ama majirani ama ndugu. Kwani mbuzi wanaongea?we nae umekuja kuaje
 
mambo bro! in short naomba nikuulize swali? before hujafunga ndoa! hulikuwa naye kwa mda gani ndani ya relationship? 2nd: mulikuwa mnaishi wote kabla ya ndoa" nyumba moja" or separete.?
 
Sawa najiskia kumpa ushauri sasa!,...........................................

Kijana mwenzangu Zungumza na Shemeji yetu...... usikae kimya.. Mwambie kwa upendo huenda yeye anajua anachofanya unakipenda. Na kumbuka kama ni ndoa ya kikristu Jitahidi sana tunaamini Mungu atasimama na wewe daima. So usimuogope na wala usiwe mkali kwake lakini mwambie tu. Kumbuka Mkeo ndo rafiki yako wa kwanza.

Haya mi nimemaliza "SWT"
 
Sawa najiskia kumpa ushauri sasa!,...........................................

Kijana mwenzangu Zungumza na Shemeji yetu...... usikae kimya.. Mwambie kwa upendo huenda yeye anajua anachofanya unakipenda. Na kumbuka kama ni ndoa ya kikristu Jitahidi sana tunaamini Mungu atasimama na wewe daima. So usimuogope na wala usiwe mkali kwake lakini mwambie tu. Kumbuka Mkeo ndo rafiki yako wa kwanza.

Haya mi nimemaliza "SWT"

hahahaha... There ur talkingHappy thanksgiving kama unasherekea
 
Mwanaume gangamala kabisa,mwambie kuwa hutaki na hupendi hiyo tabia kwisha.Wakati mwingine "mkwara"unasaidia kutatua mambo madogomadogo.
 
Aisee hiyo tabia inakera kweli...
Nina jirani yangu hapA ndio anamfanyia mume wake tabia hyo...
HatA kwenye mazungumzo unakuta jamaa anaongea bibie anamkosoa hapo hapo tena kwa mamlaka sie wa pembeni tunajiinamia...
Bi mama hataki jamaa hata asalimiane na majirani au akae na wenzie kidogo wabadilishane mawazo...
Akijaribu tu bibie anamfata...
Au we ndio jirani yangu mwe....
Cha msingi wewe ni kichwa cha familia kuwa hicho kichwa kweli..
Mweleze wazi tabia hiyo huipendi kama haelewi vitendo vinaongea zaidi.
Ila inawezekana kuna kaulegevu kwako kwenye kutimiza wajibu wako kama kiongozi wa familia...inawezekana kuna mambo ambayo kimsingi ulipaswa udhughulikie wewe lakini hufanyi hivyo na yeye ndio anafanya...hii pia inaweza kuchangia tabia hiyo....
Jikague amka be a man...a real man.
 
Aisee pole . Zungumza nae naamini mambo yatakua mazuri kwani matatizo mengi ya ndoa hutokana na lack of communication so inapoendelea for years wengi husema wanaishi kwa kuvumiliana kitu ambacho si sawa kwa wanandoa. Mweleze unakerwa na nini na kabla ya kufanya hivyo angalia kwanza je yeye ni mtu wa tabia ya namna gani sababu kuna watu ni know-it-all so watu dizaini hii yakupasa utafute namna nzuri ya kuongea nao na kuna wengine ni wanunaji so be careful.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama alivyoshauri Ablessed ongea na mkeo na umwambie vitu vyote ambavyo vinavyokukera kama ulivyovielezea hapa na kumtaka aachane navyo mara moja kwa faida ya ndoa yenu vinginevyo ndoa utaiona chungu na hata kufikia kuharibu ndoa yenu changa. Kila la heri.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom