Tabia ya watu kuniomba pesa kuwaacha wenye pesa inatokana na nini?

Shangazi yangu alishanambia kuwa ukiona watu wanakutegemea kama mzazi wao ni ishara una roho nzuri na unatakiwa kujiimarisha zaidi kiuchumi ili uendelee kupata zaidi.

Ila kumbuka tu uwe unatoa na kubakisha chako cha kukusitiri wewe na kulinda heshima yako katika jamii. Kutoa ni jambo zuri ila usitoee sanaaa hadi ukajipunja mwenyewe, hiyo si sawa. Endelea na moyo wa utoaji na ujitahidi sana kupambana ili uwazaidie hao wanaokutegemea.
RIZIKI YA WATU HUPITIA KWA WATU!
 
Utakuwa huwanyimi wakiomba kwa hiyo wanakuwa wanajulishana una roho nzuri.
 
Hili pia limesemwa humu
Ushauri wangu usiache kusaidia pale unapoweza. Ingawa aina ya kuombwa nayo ni muhimu kuzingatia mfano ninunulie bia, huo sio msaada wa msingi bali nikujitakia tu.

Iko hivi, wanaokuomba ingawa unaweza hisi wanafikiri unazo hapana, ila wanapata faraja toka kwako kwa maneno mengine wewe ni mtu wa watu. Yani wanakua na amani kukufuata wewe hata kama hauna. Labda kwa umombo ni you looks friendly to them.

Pia, usitemee kusaidiwa kifedha na hao unao wasaidia. Sie tunao amini katika imani, Mungu atakulipa kwa namna nyingine kabisa usio itarajia na wakati mwingine unaweza kuhisi ni jitihada zako, hapana. Lakini mwisho, usitarajie kwa kufanya hivyo basi utakuja kiwa tajiri - sahau. Utajiri wako wewe ni ile furaha na faraja unayoipata pale unaposaidia, ila nakuhakikishia kwenye shida zako Mungu hatakuacha.

Utajiri wa mali una mambo mengi sana nyuma ya pazia na wahusika huwa hawasemi, shukuru Mungu kwa kalama hiyo ya kusaidia wengine.
 
Nimekuelewa Sana Mkuu.
 
Back
Top Bottom