Tabia ya Wakubwa wa Majeshi yetu siku chache baada ya kustaafu kuingia ktk siasa itaisha lini???..

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Kuna hii tabia ya viongozi wa kubwa katika Majeshi Tanzania iwe Magereza, JWTZ, JTK, Uhamiaji, Polisi na wengineo kuingia kwenye siaisa baada ya kustaafu ina maanisha nini?

Na wengine walikuwa viongozi wakubwa serikalini nao baada ya siku chache wanaingia kwenye siasa hii imekaaje?

Mfano:

(1) Aliyekuwa mkuu wa Majeshi wakati huo Genenali Mboma

(2) Aliyekuwa RPC Dar es Salaam Alfred Tibaigana ambaye alimwagwa na Prof. Anna Tibaijuka

(3) Alikuyekuwa Mkurugenzi wa Jiji Bw. Mukama.

(4) Makamba baba yake January Makamba

Cha kujiuliza hivi hizo kadi za uanachama za Magamba walikuwa nazo wakati wako serikalini au?

Je, kama walikuwa na hizo kadi za uanachama ni kweli walikuwa wanawatendea haki WAPINZANI????

Manake tumeshuhudia Wapinzani wakinyanyaswa na Vyombo vya dola na isije kuwa wote ni wanachama wa magamba ndio maana wana wanyanyasa.

Angalizo: Kwa jinsi hali inavyoenda sitoshangaa baada ya Mwema kustaafu jeshi akaenda kugombea Ubunge hali inayopelekea na kutia shaka kama kweli yeye alikuwa akitenda haki.

Kumbe hawa Manjagu wengi wao ni wanachama wa magamba na huwa wana kadi kwenye mifuko yao.

Je tutafika?
 
Back
Top Bottom