Tabia ya wahudumu wa Bar kujizungusha kwenye kutoa chenji inakera

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,262
2,000
Mtu unaenda unapiga maji yako fresh baada ya kujichanga changa karibia week nzima na kubana bajeti usawa huu mbovu. Unatoa pesa unasubiri change.

Hapo ndo utaona jinsi barmaid anavyo dribble na change yako. Anajizungusha zungusha na kujichetua na change kama Bernard Morrison. Unamwona tu kuwa ni kama hana nia ya kukurudishia 2500 yako.

Mara anaenda kaunta mara anakula kona huki anatokea kule, yaani ili mradi tu akukalishe langoni mpaka ionekane ni offside.ulimwe kadi.

Hii tabia binafsi siipendi.ukimkomalia tu kidogo huku umemkazia macho unamwona anatoa change kwenye maziwa yake anakupa.wakati muda wote alikuwa akijibagaza na kuranda randa na mpira kila sehemu ya uwanja.

Hiyo 2500 si ndogo.sisi walevi inatusaidia kuondolea lock asubuhi kuanza siku nyingine. Inaondoa password then mtu unaanza ku browse upya. Haya mambo kuna siku ntamfanya mtu jambo la kinyume na maumbile. Yaani ntamtandika bakora.maana maumbile ya binadamu hayakumbwa kupigwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom