Tabia ya vyuo vikuu hapa nchini kusimamisha wanachuo kwa kipindi kisichojulikana.

Determine

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
257
79
Kumekuwa na tabia ya kuwapa wanachuo suspensions zisizokuwa na kikomo,ndani ya barua zao utakuta wameandikiwa kuwa hawatakiwi kuonekana maeneo ya vyuon hvyo mpaka wapewe taarifa zaidi,(further notes) wanachuo hao huondoka na kwenda kukaa mitaani wakisubiri taarifa hizo, wanachuo hawa hushndwa kuchukua uamzi wowote wa aidha wa kuomba kazi sehemu yoyote ile ili waweze kwa ujuzi mdogo walio nao kusaidia ujenzi wa taifa au kuomba nafasi vyuo vingne wakitaraji kuitwa ktk vyuo vyao mapema,kuna taarifa za kuaminika kuwa kuna wanafunzi wa UDOM, MUHAS na UDSM wamesimamishwa kwa muda usiojulikana, (na sasa wana mwaka mzima nje ya vyuo hvyo) ,waliandikiwa kuwa hawatakiwi chuoni mpaka watakapopewa further notes, mpaka naandika hawana further notes yoyote!wanafunzi hawa wanakaa nje ya vyuo vyao bila kujua kama watarudishwa au watafukuzwa pale vyuo vitakapowapa hzo zinazoitwa further notes,binafsi naona huu utaratibu hauwatendei haki wanafunzi hawa, make kama ni suspension wanafunzi wanatakiwa wapewe na ziwe na kikomo, kama chuo kinaamua kuwasuspend wanafunzi bila kujua adhabu zao stahili basi chuo kijitahdi kuwahoji mapema na kuwapa adhabu zao stahili mapema,yaan wanaostahili kurudishwa warudishwe mapema na wanaostahili suspension zaidi wapewe na kikomo cha suspension kiweke. Tofauti na hvyo vyuo vyetu vitakuwa haviwatendei haki wanafunzi.(source rafiki yangu wa karibu ambaye amesimamishwa )
 
ila kweli kaka sasa tuanzie wapi kuliondoa tatizo? TUSHAURIANE
 
Serikali haipo tayari kuwavumilia wahuni wachache wanaotumiwa na chadema. Kama wanapenda migomo wakaungane na kina Mbowe, ila sio chuoni. Hongera serikali.
 
Back
Top Bottom