Tychob
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 3,646
- 4,611
Habari wakuu .
Naamini Mungu ametujalia afya na uzima mbali na changamoto mbali mbali za huu mwaka.
Nirudi kwenye lengo la maada yangu . Kama wewe ni msafiri ama umewahi kutumia vyombo vya usafiri vya umma kama mabasi n.k. naamini ushakutana na hili la watu kubisha kutoa nauli iliyopangwa na inayofahamika kwa maksudi kabisa.
Mfano unaweza kua unatoka mji A kwenda mji B , na kiwango cha nauli kina fahamika kwa basi kuwa ni sh 3000. Sasa tatizo linakuja kwa baadhi ya watu, baada ya kupanda gari na pasipo kuongea na" konda "
Wakati konda anapita kuchukua nauli na anapo mfikia huyu abiria anaanza kusema "mimi nina 2000 tuu" hapo mmefika karibia nusu ya safari. Ajabu huyo jamaa anaanza kuwa mkali pale konda anamgomea juu ya hicho kiwango kinachofuata utaskia huyo abiria "ooohh mnalinga na magari yenu ,tutakua hatupandi magari yenu " cha kujiuliza wewe unapanda gari na unajua kiwango cha nauli husika . Kero ni pale linapoibuka zogo baina ya konda na huyo Abiria "msumbufu" kiasi cha kuwa kero kwa sisi wengine tunaoskiliza malumbano yao pia pale huyo abiria asiye na staha kutaka abiria wengine wamsaidie katika huo ujinga wake.
Hii tabia ipo saana kwa abiria wa nje ya miji ama vijijini na wengine.
Naamini kuna watu pia ni wasumbufu na pia kuna watu hawapendezwi na hizi tabia.
Tujifunze kuheshimu taratibu na kuheshimu kazi za watu.
Karibu uchangie chochote kama kuna kisa chochote kuhusiana na hii kadhia ulishawahi kukutana nayo...