Tabia ya polisi kupiga raia katika maandamano ya amani ni kwa maslahi ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia ya polisi kupiga raia katika maandamano ya amani ni kwa maslahi ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Nov 26, 2010.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Nov 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana jamvi,mimi bado najiuliza hili swali kila siku juu ya hawa polisi wetu wa tanzania hivi wapo ktk hiyo kazi kwa maslahi ya nani?

  kwani kila kukicha jamii inalalmika juu ya hawa polisi wetu,kwa mfano wiki hii polisi wamemkamata Mpendazoe kwa madai ya kutumia Gari la wizi,ambalo yeye Mpendazoe anadai tangu akiwa ccm amekuwa akilitumia.na amekuwa akimiliki gari hilo tangu mwaka 2007,

  mpendazoe anasema "Askari walinikamata kwa nguvu kubwa, hadi kufikia hatua ya kutishia kutumia silaha endapo ningeendelea na msimamo wangu wa kutaka kujieleza"

  Pia ktk tukio la mtoto wa mengi polisi hao hao wanalalamikiwa kwa kutaka kumbambikia madawa ya kulevya kijana huyo na walitajwa kwa majina

  Ktk kesi ta zombe ilionekana dhahili kuwa wale vijana wa mahenge walifanyiwa kitu mbaya na haohao polisi ambao kwetu sisi jamii tungedhani wangekuwa msaada kwa matukio ambayo ni hatarishi kwa jamiii

  Na hata vijana wengi niliongea nao ambao wamesha onja adha za jera walinieleza kuwa %kubwa ya vijana waliowakuta kule ni wale ambao walibambikiziwa kesi za bangi na wizi wa kuku

  Kaka yangu wa tumbo moja anayeishi MPWAPWA-DODOMA Polisi walimbambikizia kesi ya kuiba pazia kwa mkuu wa kituo Mpwapwa na baada ya siku 10 waliwakamata wahusika wakiwa na mapazia na picha za mkuu wa kituo na walimtoa kaka yangu ambaye tayari alishapokea kichapo cha hali ya juuuu


  SASA SWALI NAJIUZA NA NAOMBA WANAJAMVI MNISAIDIE HAWA POLISI WA HII NCHI YETU TANZANIA WANAFANYA KAZI KWA MASLAHI YA NANI? NANI ANAYEWALIPA KWA KAZI YA KUWABAMBIKIA WATU KESI? TUSAIDIANE JUU YA HILI

  MAPINDUZIIIIII DAIMAAAA 15202425864 :target:
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Maslahi ya watawala na mafisadi!
   
 3. k

  kuthumiwa haule Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vitendo hivi vya ukandamizaji vinaelekea kuota mizizi katika nchi yetu ,lakini kinachonitisha ni pale wananchi wanaohisi kunyimwa haki zao na kuendelea kuwa wahanga wa kuchakachuliwa maisha yao kwa maslahi ya mafisadi wachache kama makamba watakapo fikia hali ya kuwa sugu na hatimaye kuamua kusema potelea mbali, hatima ya nchi itakuwa mashakani ,je kazi ya polisi ni ipi, kama walizi wa raia na mali zao wanakua wanyanyasaji wa raia na haki zao. hili halinipi amani kabisa .:wink:
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Polisi ni adui wa raia, hiyo kauli mbiu yao ya polisi jamii haiwezi kufanikiwa kwa kuwa polisi wamekuwa wakiwatesa raia wasio na hatia, wanabambikiwa kesi mbalimbali.
  Polisi ikitaka ifanikiwe kwenye polisi jamii ni lazima wajirekebishe
   
 5. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ni tabia chafu isiyo na kifani!inatia kichefuchefu. Mwaka jana nilikuwa natembea off road pale Kibaha opposite na Kituo cha mabasi sasa wakawa wanakuja na single cabin yao mimi taratibu najitembelea jamaa walikuja wakaanza kunitukana eti natembea kama barabara ya baba yangu, na wakati wao ndio walikuwa na makosa maana ni sehemu ya pedestrians, nikasimama na sijamove basi jamaa aliileta ile ngao ya ile cabin mpaka imenigusa magoti! Mapolisi wa TZ ni wadudu wabaya wasio na values wala manners! they need to change! ni maadui wa Mtanzania.
   
 6. k

  kuthumiwa haule Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachonishangaza katika hili ni hiki , tunaambiwa RPC arusha alitoa kibali cha maandamano na mkutano tarehe 4, siku hiyo hiyo jioni IGP akatangaza kusitisha maandamano kwa kile alichokiita taarifa za kiintelijensia , swali ninalojiuliza ni hili, je taarifa hizi RPC wa arusha hakuwa nazo ila IGP pekee yake, na hao waliompa yeye taarifa hizi je hawakumpa pia RPC arusha ,na kama wana uwezo huo mbona matukio mengi ya uhalifu yanatokea bilawao kufahamu , Ukweli uko wapi Mr IGP?
   
 7. LUKAZA

  LUKAZA Senior Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 136
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Poleni mliofiwa,lakini tuliobaki tuwe na tahadhari sana na viongozi wa kisiasa.Wao wako tayari kututumia kwa namna yoyote ile ili wapate umaarufu na mslahi yao.Sasa hivi familia za wafiwa zimebaki na majonzi,lakini viongozi wa Chadema wataendelea kupeta na kufaidi mamilioni ya pesa za serikali na chama chao (Slaa mill 12 Mbowe,Lema.Ndesamburo zaidi ya mill 8 kwa mwezi)
   
 8. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Lukaza, Tatizo ni nini?
  Nawewe kagombee uongozi chadema basi
   
 9. k

  kiche JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hakuna upumbavu mkubwa kama kutojitambua!mtu anayeandika ujinga kama huu uwa ananufaika na serikali iliyopo au ni chizi tu anayeweza kuona kuwa wapo sawa!

  nchi hii ipo mikononi mwa wachache kama ilivyokuwa kipindi cha ukoloni tofauti iliyopo kipindi kile walikuwa weupe ila leo ni weusi wenzetu,maapambano ya sasa hayana tofauti na kipindi cha mkwawa,hata hivyo si ajabu kwani hata kipindi cha wakoloni wapo waliokuwa wananufaika na kuamua kuwauza ndugu zetu,wewe huna tofauti nao,machizi nchi hii wapo wengi!!!!
   
 10. s

  smartgirly Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni Riai kuuwawa bila ya sababu hii kusema akagombee uongozi Lukaza haipo sawa la msingi Chadema viongozi wake wote washtakiwe na waache kujishughulisha na siasa miaka yote ya uhai wao hawana nia njema kwa jaamii inaskitisha sana mpaka leo kuwa wapo njee viongozi wa chadema
   
 11. M

  Mnyagundu Senior Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 3, 2008
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wala sio ujinga ndio hali halisi chadema inataka kutumia maisha ya vijana wetu kwa lengo la kujitafutia umaarufu! sasa wanawapamba wale vijana waliokufa wana waita Mashujaa!!!! Ni chama cha wahuni hovyo kabisa! I hate chadema!
   
 12. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160  Jamani Polisi kwa taratibu zao, wako pale kutii amri. Asipotii amri kibarua kinaota nyasi. Ni sawa na maaskari vitani, wanatii amri kuingia vitani hata kama wanajua vita ile haina maana. Askari wa Uganda walitii amri ya Idd Amin kuvamia TZ hata kama baadhi yao walikuwa wanafahamu kuwa kuvamia nchi nyingine ni makosa. Na vita nyingine nyingi za namna hiyo zimetokea duniani na zinaendelea kutokea. Suala ni kwamba ASKARI HUFUATA AMRI YA MKUBWA WAO.

  Hata kama serikali iliyopo madarakani ikiondoka, ikaja serikali nyingine, ASKARI WATAFUATA AMRI YA MKUBWA WAO. Tofauti itakuwa kwenye nafasi ya "Mkubwa". Ina maana kuwa "Mkubwa" yeyote akiingia atawatumia ASKARI hao hao.
   
 13. m

  mzambia JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Na bado mtaijua tu kazi yetu
   
 14. m

  mzambia JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Na tutaendelea kumsikiliza mkulu wa nchi akisema kaue tunatekeleza amri ya bosi wetu mkulu
   
Loading...