Tabia ya mke wangu kuniaga 'naenda kulala', sijaipenda

ikyenja

Senior Member
May 28, 2013
103
52
Habarini wapendwa,

Kuna haka katabia ka wife sijakapenda, lakini sijui kama yupo sahihi.Kila mara ukifika muda wa kulala, hutangulia kwenda chumbani kwa kusema "naenda kulala".

Najiuliza kwa nini asiseme "twende kulala “. Mnaonaje wazoefu, wake kwa waume? Au huwa ana tatizo, lengo au maana gani ya ziada kwa kusema hivyo?

Nawasilisha.

Asubuhi na Jumapili njema
 
Huo ni uhuru tu aliokupa. haoni sababa ya kusema TWENDE TUKALALE, anaona kama atakuwa anakushnikiza, inawezekana wewe wakati huo unakuwa uko busy na mambo yako binafsi.
 
Habarini wapendm kulala “. Mnaonaje wazoefu, wake kwa waume!?

Au huwa ana tatizo, lengo au maana gani ya ziada kwa kusema hivyo!?
Nawasilisha.
Asubuhi na Jumapili njema
Mwambie awe anasema mwende mkalale
 
Sisi wanawake kuna vitu tunatakiwa kufanya tukiingia ndoani hicho ni kimojawapo.

Naenda kulala mume wangu.
(anakuaga ili kama unamhitaji muda ndio, jiongeze)

Mume wangu ninaamka (kama unamuhitaji maliza kabisa ndio aamke)

mwingine anausingizi wa karibu, mwingine akiamka hutampata tena hadi jioni kutokana na majukumu.

Kila la kheri kwenye ndoa yako
 
Asante mkuu
 
Sasa kama ana usingizi na wewe hauna!?
Sijaona kosa hapo, sijui waliooa watupe usahihi katika hili
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom