Tabia ya makondakta kukasirika ukiwapa elfu 10 asubuhi

Mwanakulipata

JF-Expert Member
Jul 17, 2018
713
1,181
Habari za usiku.

Hivi ni kazi ya nani kutafuta chenchi kati ya kondakta na abiria?

Hawa makondakta wanakuwaga na visirani asubuhi ukimpa elfu kumi anaweza akaongea hadi mwisho wa gari.

Kiukweli mimi sioni kosa la abiria kutoa elfu 10 kwasababu ni fedha halali kwa malipo ya Tanzania. Konda ndie anahitaji muda wote kutembea na chenchi kwasababu kazi yake anahitaji kurudisha chenchi.

Makondakta mwisho wa mwezi huoooo jiandaeni; ni mwendo wa elfu 10 tu

Mitano tena.
 
Kuna jamaa alitoa teni hatosahau alichofanyiwa na konda, alirudishiwa chenji coins tupu afu kawekewa kwenye condom hahaa!
 
kuna jamaa alitoa teni hatosahau alichofanyiwa na konda, alirudishiwa chenji coins tupu afu kawekewa kwenye condom hahaa!!
Halafu abiria akirudishiwa chenji za coins anakuwa mkali!!kuwa hizo hazitaki, hadi unakuwa mzozo mwingine tena!!
 
Kuna wengine wanaamua kukukomoa. Anasubiri kituo unachoshukia. Halafu huyooo! eti anaenda kutafuta chenji, kumbe yuko kobisi anasubiri gari ijae. Halafu anajitokeza: "Chengi yako hii"
 
Asubuhi chenji inakuwa mtihani kidogo kwasababu usiku wa jana yake walishaacha hesabu kwa tajiri, ni vizuri kutafuta chenji mapema ili kuwarahisishia kazi na kuondoa usumbufu
Hiyo ndio kazi yake (ofisi yake) anapaswa kuhakikisha ana vitendea kazi (chenji na tiketi) kutafuta chenji sio jukumu la abiria hilo ni jukumu la mtoa huduma ya usafiri. Ukiingia kwenye hiyo biashara unapaswa kutegemea fedha za aina zote, hivyo unapaswa kuwa na chenji kwa wateja wako hakuna mjadala kuhusiana na hilo.

Ni kukosa ustaarabu tu na kutojielewa kwa wanaotoa huduma ya usafiri ndiko kunakowafanya kukasirika wakati ni jukumu lao.

Lugha chafu kwa abiria, uchafu wa mabasi ya abiria, kukatisha ruti, kujaza abiria kuliko idadi inayotakiwa ndio jambo linalofanya watu kukopa magari.

Public transport hapa nchini ni mbovu Sana na kwa bahati mbaya Sana hakuna anayejali kwakua wanaopaswa kujali tayari wanausafiri binafsi.
 
kuna jamaa alitoa teni hatosahau alichofanyiwa na konda, alirudishiwa chenji coins tupu afu kawekewa kwenye condom hahaa!!
Huo sasa ni ulimbukeni sio sifa.

Inashangaza Sana jamii yetu kuwa na watu wa aina hii ambao wanafanya mambo ambayo sio ya kiungwana kabisa lakini ndio wanaonekana werevu.

Unaweza ona huyo konda ni mtu wa aina gani.

Badala ya kustaarabika tunazidi kuwa wajinga kupitiliza.
 
Hiyo ndio kazi yake (ofisi yake) anapaswa kuhakikisha ana vitendea kazi (chenji na tiketi) kutafuta chenji sio jukumu la abiria hilo ni jukumu la mtoa huduma ya usafiri. Ukiingia kwenye hiyo biashara unapaswa kutegemea fedha za aina zote, hivyo unapaswa kuwa na chenji kwa wateja wako hakuna mjadala kuhusiana na hilo....
Kabisa mkuu, kuna uovu mkubwa ila hausemwi tu.
 
Mara nyingine Hekima ituongoze, usione kuwa ni fedha halali kufanyia malipo ikawa ndio fimbo ya kumkomolea. Ile ni kazi kama wewe uendavyo kazini kwako.

Litafakari hili,

Upo dukani kwako asubuhi, halafu mtu anakuja kununua kitu cha shilingi mia tano asubuhi na mapema akakupa elfu 10.
 
Mara nyingine Hekima ituongoze, usione kuwa ni fedha halali kufanyia malipo ikawa ndio fimbo ya kumkomolea. Ile ni kazi kama wewe uendavyo kazini kwako....
Ile ni ofisi kaka labda nikuulize swali, ni kazi ya nani kutafuta chenchi kati ya abiria au kondakta? Yaani mimi nimerudi kutoka kazini usiku nianze kutafuta chenchi kwenye maduka.

Yeye konda anajua kabisa kazi yake inahitaji chenchi inakuaje habakishi kidogo kwaajiri ya kuanzia kesho.

Huu ni uzembe, mbona tukienda dukani hatuendi na chenchi kamili?
 
Ile ni ofisi kaka labda nikuulize swali...ni kazi ya nani kutafuta chenchi kati ya abiria au kondakta?... Yaani mimi nimerudi kutoka kazini usiku nianze kutafuta chenchi kwenye maduka..
Soma tena nilichokiandika unielewe, mara zote ongozwa sana na Hekima kuliko Haki kama unavyojinasibisha na maisha yako yatakuwa mazuri mno.
 
Kuna logic yao inanichekeshaga sana.

Mtu mzima akimpa 10,000 anatakiwa arudishe chenji 9,600(kwa nauli ya 400), Hapo hasemi kitu

Aje sasa mwanafunzi na sh500 tu (ambapo chenji ni 300) tu ,konda ataropoka hadi mwisho wa safari 🤣🤣
 
Back
Top Bottom