Tabia ya Makondakta kuita abiria Mawe

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Wanabodi,

Naomba niwasilishe mada hii kwenu kama kichwa cha habari kisemavyo.

Kadri siku zinavyoenda naona hii tabia ya makondakta wa mkoa wa Dar na mikoa ya jirani wamekuza hili neno "mawe ' kwenye kuwaita abiria ambao hawashuki kwenye vituo vya karibu mara baada ya bus kuanza safari.

Nimekereka sana pale unapotoa nauli yako cash, mfano unatumia bus la ruti ya CHANIKA - SEGEREA nauli pale ni 450 au 500 sina uhakika.. utakuta abiria kapandia Chanika anasema mwisho wa bus Tabata Segerea labda ndio ka kibanda Kake ka kazi kapo hapo basi njiani utakuta ni masimango matupu, mara 'ooh nimebeba mawe leo hayashuki','ooh dereva tembea mpaka Segerea hawa wamekodi leo " na kauli nyingine sizizo za kistaarabu.

Sasa swali je hiyo nauli iliyochajiwa na kupangwa na serikali mfano kama kutoka Gongolamboto - kivukoni kama ni 500 haiwatoshi???

Kama abiria Amepanda bus Lako na katoa nauli full lakini hajafika kituo anachoshuka let's say ni mwisho wa gari kwa nn mnakua mnatoa maneno ya shombo???

Kwani nauli si kawapa ya kipande husika??,kwa nn mumseme????

Basi pandisheni hiyo nauli iwe 700 ili muwaache abiria wanaotoka mwanzo wa bus na kushuKa mwisho wapande kwa raha zao na wa enjoy nauli yao.

Kwa nini Makonda mnakua selfish, mnaona wao (abiria) wanatakiwa kupanda na kushuka ili mupandishe abiria wapya wawape pesa zaidi. Badilikeni hii sio haki.

Mbona wenzenu wa mabus Ya mkoa mfano arusha - dar kama abiria wakilipia nauli pale shekilango kwenda arusha hawana masimango njiani? Ndo kwanza wanawapa vitafunwa (refreshments)..sababu wanaheshimu mkataba kwamba abiria katoa hela yake basi AHESHIMIWE.

Same apply kwa usafiri wa daladal, abiria katoa nauli full basi AHESHIMIWE, mteja ni mfalme usianze kumkashifu kwa kumuita abiria wa leo ni MAWE.

Wakati mwingine mnajifanya Hamtaki kuchukua abiria kituoni bus linapoanzia kwa kigezo kwamba abiria wanaosubiri bus kituo cha mwisho huwa hawashuki.

Sasa mnataka abiria wakasubirie bus wapi kama sio kituoni?

Na wangekua hawashuki si wangekua wanalala kwenye mabus yenu.

Heshimuni abiria na abiria wawahesimu.

Hasa nyie mnaovaa tisheti zenu za UWAMADAR.

Badilikeni mpo kazini. Yale mabus ndo ofisi zenu na sisi ndo wateja.

Naomba kuwasilisha.
 
Ndugu yangu hayo ndio mambo ya Public transport

Huwezi yapata kwenye Uber, taxify wala bolt, ni kuyazoea tu

Mzee kuna majina wale wa NYUMA, WA MBELE

Wakati Mwingine huwa wanaleta burudani katikati ya kuchanganyikiwa kwa abiria hao hao.
 
Ndugu yangu hayo ndo mambo ya Public transport,
Huwezi yapata kwenye Uber,taxify wala bolt,ni kuyazoea tu,
Mzee kuna majina wale wa NYUMA,WA MBELE,
Wakati Mwingine huwa wanaleta burudani katikati ya kuchanganyikiwa kwa abiria hao hao..

Utamsikia konda nyie wazee hapo nyuma mtanipa? Na nyie wakina mama hapo mbele mtanipa?
 
Miaka nenda miaka rudi, makondakta wamekuwa na lugha chafu juu ya abiria. Imekuwa kama ni tatizo la kimfumo hivi na ambalo abiria na mfumo wa usafirishaji umelikubali.
 
Twende taratibu! Mfano;
Coaster ya diesel kutoka Masaki hadi Ubungo ni km 15.
Abiria wakijaa level seat unapata 10,000
Unatumia mafuta kati ya 5,000.
Faida ni inakaribia au inazidi 5,000 na mgawanyo wake tukigawa sawa kwa sawa ni kama ifuatavyo;
Mimi napata 1,250
Dereva anapata 1,250
Tajiri anapata 1,250
Gari linapata 1,250
Pia kwenye faida hiyo hiyo ya 5,000 trafiki anataka chake (hela ya chini ni buku mbili (2,000)
Sasa kwa ruti ambazo hazina abiria wengi tukionaga wamekaa wa mwanzo mwisho, vichwa huwa vinauma.
Kuna kipindi nilikuwa konda wa parttime nilimpiga kichwa abiria nusura azime.
Kila kituo alikuwa anamwamrisha dereva asisubiri abiria kwa sababu ni muda wa kazi anawahi, dereva akawa anatii.
Tumefika Magomeni angalau nizibe mapengo akawa anamwamrisha tena, nikamwambia mzee unapopanda daladala manake umekubali vigezo na masharti yake, ambapo humu abiria wote tunachangia 400 na nikifika kituoni nasubiri abiria....
Kufupisha stori akanipiga kofi eti nitafute kazi za maana. We! We! We!
 
Back
Top Bottom