Tabia ya mabinti kuwafanya Boyfriends zenu baba or walezi wenu

acha kulialia kama huna pesa kaa pembeni. waache wenye pesa wanaojua kuhonga wafaidi vitu. mwanamke anataka pesa bwana sio suruali yako tu
 
Hayo ndugu zangu ni matatizo ya malezi wanayopewa hawa mabinti kwao. Nakumbuka nikiwa mdogo mama yetu alitulea kuwa ni MARUFUKU kuomba ela kwa mtu yeyote zaidi ya wazazi. Lakini nilikuwa nashangaa kuna mtoto wa jirani yetu kabinti kazuri na kwao mambo safi, yani yeye alikuwa ni kama wimbo "SHIKAMOO NAOMBA ELA" hata kwa wapita njia wazazi wake badala ya kumpa kichapo wanakenua tu. Sijuhi sasa hivi yuko wapi but am sure atakuwa sampuli hizo za kufanya wanaume ATM.

Tuwalee watoto wetu kuwa independent otherwise watatumiwa na wanaohonga magari MEKUNDU.

Huwa Naepuka sana kutoa pesa kwa watoto waliovaa uniform pale wanaponiomba. Unaweza kumpa leo, kesho akaomba kwa mtu ambae ni paedophile akidhani ni kawaida kwa watoto kupewa pesa na wapita njia akavutiwa chumbani na kubakwa N.k Najaribu kupambana na hilo ili watoto wawe salama. Zamani Nilikuwa Nikigawa sana pesa kwa watoto lakini Nilipoona visa vya udhalilishaji wa watoto vikiongezeka, Nikaona Nijaribu kuanzisha vita dhidi ya hayo matendo kwa style ambayo ni independent.
Kwa upande wa wanawake, kuhongwa sio kitu cha ajabu ila wakati mwingine iko so demeaning. Kuna vitu vya kuomba lakini vingine vinakufanya uwe mtu wa kutawaliwa kwa vile unaonekana cheap. Imagine kila siku unaomba luku, hela ya saloon, lunch, vocha, nauli n.k Na huzungumzii kuomba kufunguliwa mradi wowote utakaokuwezesha kujitegemea au kila unapopewa mtaji unaula na kurudi kuomba tena, hiyo ni dalili kuwa wewe una tatizo linalohitaji ufumbuzi na si kukomaa na madai kuwa mwanaume ndie tu anaepaswa kukuhudumia. Ingekuwa hivyo kusingekuwa na wakina mama wenye biashara zao kubwa tu.
Kingine ni kuwa kuhongwa hakumfanyi mwanamke awevna mapenzi ya dhati na ndio maana wapo wanaohonga mpaka wanafilisika lakini bado wanaachwa na pia wapo wasiohonga au kuhonga kidogo wanadumu kwenye mahusiano yao. Hili hata wanawake mnalijua, mtu anaweza kuwa anakupa vingi lakini bado unamuona ----- tu na moyo wako uko kwa mwehu mmoja ambae hana time kabisa na wewe. Sasa kama kuhonga hakujengi uhusiano, mnakung'ang'ania kwanini? Jibu kuu ni moja, mahusiano ya kuhongwa yako kimaslahi zaidi.
Mwanamke anaejitegemea, anaeishi kwa juhudi zake binafsi, hawezi kulilia kuhongwa sana. Atataka zawadi tu lakini si kutegemea kuhongwa ndio kumfanye apende.
 
inategemea aina ya wasichana mnaowatongoza.wengine mnawatongoza kwa ajili ya game tu,na wao wanaona bora wajinufaishe mapema.au wengine mkitongoza mnajisifia tuuuu,wakati uwezo huna ni kama gia tu ya kuingilia.msiwalaumu,makosa ni yenu wenyewe.

Bora wewe umesema la maana. Unakuta mtu hajui mapenzi ni nini, mwanamke anataka mazungumzo gani ili kumuinterest, au hata awe na hamu ya kuendelea kukusikiliza, unakuta mtu kazi kujisifu kama toto la Nursery;Nimeagiza fortuner Japan, Najenga Kimara, Ukinikubali Nitakujengea, Nitakununulia gari n.k Obviously ukikubaliwa, kitakachokuwa kimeleta mvuto ni ahadi na matumaini ya alietangaziwa kuwa atakuchuna, ndio maana utahonga sana lakini hataridhika mpaka uishiwe akuache.
Na kipindi anapokuchuna, anatafuna na mtu mwingine. Inakera sana.
 
Duuh si msitoe tu hizo hela jamani, mtu unalalamika weee utadhani umeshikiwa bastola bana Kwamba utoe kilazima eeh.
 
Nyie wanaume mnapenda vitu vizuri. demu apendeze, anukie, nywele nzuri, ukituma msg akujibu na mambo mengine kibao. Sasa vyote hivyo vinagharimu pesa. Mwanaume unatakiwa kuwajibika..ht km sio mkeo ni wajibu wako. Yaani ipo hivyo tu mkatae au mkubali.

Sawa kuna wadada ambao wamezidi kupiga mizinga. Lkn wewe Kama mwanaume unatakiwa kuwajibika bila hata kuambiwa. NDO HIVYO YAANI.
 
ukiwa nacho mpe ukiwa huna mwambie huna!kama ni mwelewa atakuelewa kama sio mwelewa hatakuelewa
 
Nyie wanaume mnapenda vitu vizuri. demu apendeze, anukie, nywele nzuri, ukituma msg akujibu na mambo mengine kibao. Sasa vyote hivyo vinagharimu pesa. Mwanaume unatakiwa kuwajibika..ht km sio mkeo ni wajibu wako. Yaani ipo hivyo tu mkatae au mkubali.

Sawa kuna wadada ambao wamezidi kupiga mizinga. Lkn wewe Kama mwanaume unatakiwa kuwajibika bila hata kuambiwa. NDO HIVYO YAANI.

kwani mi babaako
 
Back
Top Bottom