Tabia ya kushika / kuchungulia simu za waume / wake zenu muache!! Ohooooo

Mi pia,
coz hata nisipofanya ukaguzi bas nakaguliwa mimi!
Na nafanikiwa, karibu katika kila ukaguzi wangu nabamba uozo!
so nakua najiupdate!

mmh...wewe una bahati....sijawahi kubamba hata siku moja.......sijui ni ujanja gani unatumika hapo.......
 
ni bahati....ukikuta si ndipo unapoanzia.......

Kweli napataga pa kuanzia,
ila huwa sikaguagi tu from no where
nakuaga nishahisi kitu nakifatilia ndo nakibamba
sasa hapo katika kufatilia kimoja nagundua vingine kama kumi hivi
ndo napodataga...
nashindwa hata nianzie wapi sasa!

Nashukuru huwa sina pressure
vingine napotezea,vingine naanzisha msala
halafu maisha yanaendelea!
 
Kukagua thimu muhimu best, binafsi mwanzoni nilikuwa naikagua na yeye akiwa anaona ila nikagundua inamkera kweli, yaani hapendi kabisa. Siku hizi najifanya sina time na simu yake ila nikivizia kaenda kuoga tu ninayo kuanzia kwenye Inbox, Sent Items mpaka kwenye cal log, nione ni simu gani imepigiwa, imepiga na pengine haikupokelewa na ni muda gani? abiria unachunga mzigo wako bana.
 
Hahahahaaaaaa! Kuna mtu kanichekesha huku ofisini, anadai kapata dawa ya ukaguzi wa simu!!!! DAWA NI KUWA NA SIMU MBILI TUUUU! Moja ya magumashi, invitation to treaties, nyumba ndogo,n.k yalala ofisini au kwa droo ya gari, ingine ndo yaingia nyumbani. Ya nyumbani majina yale yale MAMA, SHANGAZI, BAMDOGO, SHEMEJI, ALFRED OFISINI, JUMA SITE, MCHUNGAJI JOHN, BOSI IDDI, SEKRETARI LINDA!!!! Akifika anaiweka kwa meza incase ukijisikia kukagua!!! LOL! Sio kwamba mie sikaguagi, nakagua sanaa ila sasa itabidi nitafute inside information TIGO na VODA amejisajili LINE NGAPI!!!! LOLEST!!!!
 
Amani kwenu wakuu! (Wakubwa Shikamooni)

Leo ujio wangu si wa Verse moja nyingi Baba V LOL!

Kweli ile tabia ya kuperuzi na udadisi simu za patner wenu muache!!! Tena unakuta mtu anatime mwenzie anaoga anafanya thera checkup ya simu kuanzia inbox, outbox, call log, sms counter(incase zilifutwa), emails na call time summary. Hapo unakuta kakunja nne kabisa, kinotebook mkononi na juisi pembeni, kwa raha zake.

Mwenzenu Mamushka mmoja lilimkuta la kumkuta kati kati ya kuperuzi na kudadisi, Mumewe kufika kaingia chooni, yeye si akazama kunako koti na kukitia kilongalonga kunako 18 zake maoja kwa zote kwenye sms si ndo kukuta huu ujumbe!!!!

"BWANA MKWE FANYA UTARATIBU UTAFUTE NJIA ZA KIDIPLOMASIA KUMWAMBIA MKEO KUWA MAMA YAKE AMEFARIKI GHAFLA LEO MCHANA HUKU KIJIJINI, NA MFANYE UTARATIBU WA KUJA MAZISHINI!!!! UTAFUTE UJANJA WA KUMWAMBIA SABABU ANA PRESSURE KALI SANA YULE SI UNAJUA, HATA SISI HATUJAMWAMBIA NDO TUNAKUTEGEMEA!!!!"

Kilisikika kishindo tu cha Mtu kudondoka na pressure!!!!

SMTMS ITS NOT WORTH IT!!!!!.

Hivi akishakua mume wako kwani kuna mambo gani ya ziada ya kufichana mpaka simu iwe ya kwako mwenyewe??ama sababu tumeshajijengea wizi mtupu mpk kwenye ndoa ndo mana mtu unakua hauko huru na simu ya mume ama mke aishike,,,Mi natamani sana tuwe na open relationship hasa mkishaingia kwenye stage ya ndoa ama uchumba,kua free kwa lolote ambalo unataka kujua kwa mwenza wako,si ni mume jamani kwani ni mpitanjia??
 
Last edited by a moderator:
Mimi yalishanikuta makubwa kwa ajili ya kuchunguza simu ya hubby ila sijaacha na siachi ng'ooo,maana naona hiyo ni mojawapo ya haki zangu za msingi,na akitaka timbwili aweke password mpya nisiyoijua!!
 
Hahaha, leo!
Sina mbavu hapa. Wenzio tuna uzoefu wa investigation. Nikiona msg ya msiba silii wala nini na najikausha kama sijaona (ili tusijadili financials hehehe). Na simu za kisasa unaclick 'mark as unread'. Akiniambia twende kwenu nasema sina hela. Nadeeka afu ndo nalia. Kama unaona msg ya kuibiwa na unakaa kimya unafanya maamuzi, seuze msiba lololo
 
Akiweka password wala usimuulize, weka na wewe yako password hadi akiiweka kwenye charger itakiwe password. Wanajidai hawaangalii ila ujue ukilala anaangalia. Tofauti ni kuwa mie naangalia hadharani, mbele yake! Unajificha kwani small house hiyo? Eboo!
Mimi yalishanikuta makubwa kwa ajili ya kuchunguza simu ya hubby ila sijaacha na siachi ng'ooo,maana naona hiyo ni mojawapo ya haki zangu za msingi,na akitaka timbwili aweke password mpya nisiyoijua!!
 
hapana kwakweli me mambo haya ya kumkagua mtu niliapa i will never do it.nashangaa sana wanawake wenye pressure kama hizi ivi ina maana unatafuta kuugua pressure au kufa mapema??then umuachie nafasi huyo mwizi wako afaidi??tabu ya nini bwana me haya mambo ya kukagua simu hapana.kuna dada mmoja my work mate eti yeye anampaka mtu sever room ya mtandao mmoja wa simu yan kazi yake kupewa feedback tu kuwa mme wake yuko maeneo gani hadi amekonda kwa pressure.kutafuta maradhi tu!
 
daima mimi ni muumini wa ukweli na uwazi,mke wangu ana haki ya kuchungulia simu yangu apendavyo...kwa kweli simu yake si kwamba nachungulia bali naangalia..mara nyingi jioni nachungulia jf kwa simu yake,mi natumia simu ya tochi haina intaneti so nipo huru nayo,na msg zikiingia wakati naperuzi jf huwa ananiambia nimsomee.siku nyingine anaweza kusahau simu zake ananiambia niende home nikamchukulie

nami siku nyingine naenda ktk umc nimesahau simu yangu yeyote namuuliza kama ipo home ananiambia ipo basi naendelea na kusherehesha mpaka narudi home,kifupi kama hauna mawaa suala la simu yako kukaguliwa au kuangalia its nothing
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom