SoC01 Tabia ya Kupiga Wanawake Kwenye Mahusiano Ilaaniwe Kwa Nguvu Zote

Stories of Change - 2021 Competition

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
974
1,525

Tabia ya Kupiga Wanawake Kwenye Mahusiano Ilaaniwe Kwa Nguvu Zote
Kupigana na mwanamke au kupiga wanawake kwenye mahusiano ni tabia inayokera, inayoashiria hatari na kuleta maumivu mengi ya kimwili na kihisia sio tu kwa muathirika anayepigwa, bali hadi kwa ndugu na jamaa wanamzunguka na jamii kwa jumla. Tabia hii ya kupiga imekithiri zaidi kwa wanaume huwapiga wanawake, ingawa kuna idadi ndogo ya wanawake wanaowapiga wanaume. Hili la wanawake kuwapiga wanaume hakijazoeleka sana kama ambavyo wanaume wanavyowapiga wanawake. Tabia hii imezoeleka kiasi cha kuwafanya wenye tabia ya kupiga kuona kana kwamba ni haki yao kufanya hivyo.

Vyombo vya habari kila kukicha vinaripoti matukio ya wanawake kupigwa na kupata madhara yanayowaletea athari za muda murefu kwenye mahusiano na maisha yao.

Mfano mmoja ni kisa kimoja ambapo mwanamke mmoja huko kaskazini mwa Tanzania aliyepigwa na mumewe hadi kukatwa kiganja cha mkono wake, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Lengo na mume huyu lilikuwa kumpiga mkewe, kumkatakata hadi kumuua. Laiti kama isingekuwa majirani waliowahi kuja kumuokoa mwanamke huyo, leo hii angeshakuwa marehemu. Mama huyo wa watoto wawili ambaye inasemekana ni mwalimu kitaaluma, amenukuliwa akisema kwamba kinachomsikitisha kuhusu kupoteza kiganja chake ni kwamba hataweza tena kufanya kazi yake ya ualimu iliyokuwa ikimuingizia kipato kilimchomsaidia yeye mwenyewe, watoto wake, wazazi na ndugu zake. Kosa baya kiasi gani alilofanya mama huyu hadi kuadhibiwa kiasi hiki? Unaweza kujionea mwenyewe kiasi gani athari za kupigwa mama huyu zilivyo mtambuka. Natamani kumsikia mume aliyefanya unyama huu naye aje aseme sababu zilizomfanya kufikia uamuzi wa kinyama kama huu.

Visa kama hivi vya wanawake kupigwa si vigeni masikioni mwa watu wengi

Kumpiga mwanamke ni tabia isiyo ya kistaarabu, ni ujinga, ni kosa kisheria, ni unyama na pia ni aina fulani ya ukatili wa kimwili unaopaswa kulaaniwa kwa nguvu zote. Kinyume cha unyama ni ubinadamu, hivyo mwanaume mwenye ubinadamu ni mstaarabu hivyo hapaswi kuwa na tabia ya kinyama ya kupiga mwanamke.

Mara nyingi hustaajibishwa na sababu au visingizio vinavyotolewa na wanaume wenye tabia ya kupiga wanawake. Kuna baadhi ya wanaume wana tabia hii kwa ajili ya kufuata mkumbo tu, hata ukiwauliza hawana majibu yoyote ya maana, lakini kuna wengine kupiga kwao ni tabia ya mazoea iliyokithiri na hata huona fahari kufanya hivyo.

Maswali yafuatayo yanaweza kumfanya mwenye tabia ya kupiga mwanamke ajitafakari

Kwanini unampiga mwanamke?
Huenda atajibu; Huyu mwanamke ni mkorofi, amekosea, amenikosea, hana adabu, anataka kunipanda kichwani na mwisho watasema, ‘nilikuwa na hasira tu’, n,k.

Huyu angekuwa ni binti yako, dada yako au mama yako mzazi, kwa kosa alilofanya unadhani anastahili kupigwa?
Wewe unayepiga kwani huwa hukosei, na je ukikosea nawe upigwe?

Mwanaume mwenye tabia ya kupiga mwanamke anapaswa kutafakari kwamba tangu amekuwa mtu mzima ameshafanya makosa mengi na pia amewakosea wengi maishani mwake. Akiwa kazini au kwenye shughuli zake pia ameshafanya makosa mengi. Je, makosa yote aliyoyafanya naye anapaswa apigwe?

Baadhi ya sababu zinazosababisha wanaume kupiga wanawake

a) Hasira ya kukosa uwezo na ushawishi wa kujenga hoja

Kwa wanaume wengi, tabia ya kupiga ni njia ya mkato baada ya kushindwa kwa nguvu ya hoja, hivyo njia rahisi kwao ni kupiga. Mara nyingi kunakuwa na hoja mezani inayohitaji majadiliano na kufikiwa uamuzi, na kwenye majadiliano kuna uwezekanao wa kuwepo kwa maoni na mawazo tofauti, hivyo ili maamuzi yapitishwe unahitajika uwezo na ushawishi wa kujenga hoja, hata wenza wanapozungumza huenda wakapaza sauti juu, au kuwepo na ukali na jazba kujitokeza, lakini hatimaye kinachoshinda ni nguvu ya hoja. Kama huna nguvu ya kutetea hoja yako kimantiki, ina maana hutashinda mjadala, matokeo yake inabidi mwanaume atumie nguvu kwa njia ya kipigo, ili aidha kuufunga mjadala au alazimishe suala lake lipite kwa nguvu.
Kwa hasira, kwa kuwa mwanaume mwenye tabia ya kupiga anajikuta hana uwezo wa kujenga hoja, hivyo anatafuta njia ya mkato ya kutatua hilo tatizo, hivyo anaamua kutatua tatizo kwa nguvu… kwa kupiga.

Jaribu kufanya utafiti wako mwenyewe binafsi, utagundua kwamba wanaume wengi wenye tabia ya kupiga wanawake, hawajiamini, hawana uwezo na ushawishi wa kujenga hoja, badala yake wanatumia njia ya mkato ya nguvu ya kupiga. Mwanaume anayejiamini, mwenye uwezo wa kujenga hoja, ana sababu gani ya kumpiga mwanamke, tena wakati mwingine ni mwanamke anayempenda?!

Wanaume wenye tabia ya kupiga wanawake wanapaswa wajifunze kufikiri vizuri, wajiamini, wajifunze kujenga hoja, kushawishi kwa upole na upendo, kwa hoja na si kwa kutumia nguvu.

b) Uwezo na matumizi mabaya ya nguvu zake za kimwili
Kimaumbile mwanaume ni kiumbe aliyejaaliwa nguvu za kimwili zaidi kuliko mwanamke, mwili wake wa kawaida ni mkubwa kulinganisha mwanamke, hata wakati mwingine kufikia kuwa na mwili mkubwa zaidi kuliko hata mwili wa mama yake mzazi aliyemzaa. Hali hii kwa baadhi ya wanaume, humpa kiburi na uhakika wa kumshinda mwanamke kwa nguvu za kimwili. Lakini wanaume na wanawake wangekuwa na nguvu sawa za kimwili, vipigo dhidi ya wanawake vingepungua sana.

Hali hii imeifanya hata jamii kutafisiri kwamba wanawake kuwa dhaifu, hata baadhi ya watu hupendelea kuwaita wanawake kwamba ni ‘viumbe dhaifu’, hebu kwa mfano tukubaliane na msemo huu kwamba ‘wanawake ni viumbe dhaifu’. Kwa jinsi ninavyofahamu, kiumbe dhaifu hakina uwezo wala nguvu ya kufanya chochote, mfano mtoto mchanga, bibi kizee, mgonjwa au mtu ambaye hana nguvu na hawezi kujitetea. Hivi kweli ni sahihi kumpiga kiumbe dhaifu kama mtoto mchanga, bibi kizee na hata mgonjwa? Sasa mwanaume mwenye nguvu zote hizi, anawezaje kutumia nguvu zake kukipiga ‘kiumbe dhaifu’ (mwanamke), wakati akijua wazi kwamba kiumbe hiki hakina nguvu zaidi yake? Unadhani nani hapo ni dhaifu?

Wanaume wenye tabia ya kupiga wanawake wanapaswa kutambua kwamba kuna maeneo nguvu zao za kimwili zinahitajika sana kuliko kuzifuja kwenye mwili wa mwanamke, ni bora kupeleka nguvu hizo huko, zinakohitajika kama shambani, kwenye kuchimba mashimo, kubeba mizigo mizito, tena kwa kulipwa ujira kwa kuzitumia nguvu hizo vizuri, lakini si kwa kumpiga mwanamke.

Kamwe usitumie nguvu hizo kwa mwanamke ambaye umeweka kiapo kwamba utampenda, utamlinda na kuishi naye kwa shida na raha maisha yako yote. Mwanaume anapaswa kutambua kwamba kama ana tabia ya kupiga wanawake basi yeye ndiye dhaifu na si mwanamke, na kwamba wenye nguvu huzitumia nguvu zao kwa kujenga hoja na si kwa kupiga wanawake. Pia kumpiga mwanamke ni kosa la jinai kwa sheria za nchi, na anayo haki ya kwenda kushitaki mbele ya sheria, asipokwenda basi ujue kwamba ameamua tu kuchagua kusamehe.

c) Mila, desturi na imani za msingi
Kuna baadhi ya wanaume wamejijengea tabia ya kupiga wanawake kwa sababu za kimapokeo na sehemu ya mila na desturi za utamaduni wao. Tangu wamezaliwa, kwenye malezi na makuzi yao wamekuwa wakiona kuwa ni jambo la kawaida mwanaume kumpiga mwanamke. Kwa sababu baba alikuwa anampiga mama yake, kaka mara kwa mara amekuwa akimpiga mke wake, hivyo naye anaona kwamba hilo ni jambo la kawaida na fahari kwa mwanaume kufanya hivyo. Nyakati zimebadilika, nasi kama wanadamu tunapaswa kubadilika kuwa wastaarabu na kuachana na mila zinazodhalilisha utu wetu. Pamoja na kwamba tunapaswa kulinda, kuheshimu mila na desturi zetu, ni muhimu kupima kama kuna faida kweli ya kuendelea na baadhi ya mila fulani hizo kwa nyakati hizi.

Tunawasaidiaje wanaume wenye tabia ya kupiga wanawake?

Zifuatazo ni baadhi ya mbinu zitazoweza kumsaidia mwanaume kuepuka tabia ya kupiga wanawake.

a) Tambua kupiga si suluhisho na hakutatui tatizo
Sehemu ya kwanza inayofanya maamuzi ya kupiga ni akili yako, hivyo iambie na iaminishe akili yako kwamba hutapiga tena, kwani kupiga si suluhisho na hakutatui tatizo, bali hujenga hofu na kuondoa upendo. Usichanganye kati ya hofu na upendo. Kwa mfano wewe umerudi nyumbani leo umechelewa na umekuta chakula hakijawa tayari. Unaamua kumpiga mwenza wako kwa sababu ya kuchelewesha chakula. Siku inayofuata utakuta chakula kimeshaandaliwa kwa wakati, ukidhani kwamba sasa unapendwa kwakuwa tu leo chakula kimewahi, kumbe ulichokijenga kwa mwenza wako ni hofu na si upendo. Kipi ni bora kujenga kwenye mahusiano, upendo au hofu?

Kwa mfano, mwenza wako huenda hajisikii kushiriki tendo la ndoa pale wewe unapohitaji, na kwa tafsiri yako amekunyima, hivyo unaamua kumpiga au kumlazimisha bila ridhaa yake. Siku nyingine atakubali kushiriki kwa sababu tu ya hofu uliyoijenga na si upendo. Tambua kuna tofauti kubwa ya mazingira kati ya chakula kilichoandaliwa na mwenza wako kwa upendo, na kile kilichoandaliwa kwa hofu, vivyo hivyo mazingira ambayo mwenza anayeshiriki tendo kwa upendo, na pale anaposhiriki kwa mazingira ya hofu au kulazimishwa.

Kusikilizwa na kuheshimiwa na mwanamke kwababu ya upendo wake kwako, ni tofauti sana na kusilikizwa na kuheshimiwa na mwanamke kwasababu ya hofu yake kwako. Mwanaume unapaswa ujiulize kipi ni bora kuwa katika mahusiano yanayojengwa kwa misingi ya upendo au misingi ya hofu? Jibu nakuachia wewe.

b) Epuka kufanya maamuzi ukiwa na hasira
Ukijihisi una hasira au umekwazwa kwasababu zozote zile, jaribu kutozungumza sana na usifanye maamuzi yoyote kwanza, ikibidi ondoka eneo la tukio na uende mahali pengine ili ubadilishe mazingira na upate fikra tofauti. Jipe muda kabla hujafanya jambo unaloweza kulijutia baadaye. Kwa mfano uko chumbani mmetofautina na mwenza wako, toka chumbani na hamia sebuleni, au toka nje ya nyumbani kwako kabisa, nenda kajipatie kinywaji chepesi maeneo ya jirani, au fanya matembezi mafupi mitaa ya jirani, kuliko kupiga, kumbuka unapompiga mwanamke hutatui tatizo la msingi, bali unaongeza tatizo.

c) Vaa viatu vya mwanamke anayepigwa
Jenga taswira kwamba huyu mwanamke unayetaka kumpiga ni mtu wako wa karibu anayekuhusu, kwa mfano binti yako, au dada yako au mama yako na wewe ni yule mwanaume anayetaka kumpiga. Sasa je, unaona kwamba huyu binti yako, dada yako au mama yako anastahili kipigo? Ukijaribu kutafakari kwa njia hii utalitazama suala la kumpiga mwanamke kwa mtazamo tofauti kwamba si sahihi. kumbuka mwanamke ni mtu wa kupendwa, kujaliwa, kuongozwa na si kupigwa.

Dunia na mazingira yake yanabadilika, nasi pia tunapaswa tubadilike

Nawasilisha
 
Tunapigana baada ya hapo tunakwenda kitandani kuombana msamaha.
NB; Hatusababishiani majeraha...tunatoana hasira tu na jasho.
 
Ujinga tu.hawa wanawake wa Sasa hivi bila makofi ya hapa na pale ndoa haiendi.

Yote ni kwa sababu wazazi wa siku hizi wanabweteka mitoto inashinda kwenye makatuni matokeo Hadi kwenye ndoa yanaishi Kama makatuni
 
Tabia ya kuwatukana na kuwadharau wanaume ipingwe na wanaume kwa kuvaa viatu vyao na kukaa kwenye nafasi zao sawasawa.

Kupigana ni ukatili wenye ushamba mwingi sana. Mwanaume anayempiga mwanamke ni mwanaume asiye na uwezo wa kutatua matatizo kwa kutumia akili zake

Muishi nao kwa akili sio kwa kuwapiga
 
Asante
 
Jana nimetoka kazini amejisaidia/kajititia namwamwambia umtoe,kasema Kwan we huwez kumtoa? Nikajibu naweza mbona namtoaga siku zote saiz nataka niondoke Tena.kajibu Kama humsafishi mwanao utajijua Kwanza pengine unamsaidia kumlelea mwingine
 
Mkuu kama bado unampenda piga vichwa umung'oe hata meno mawili.

Kama umelichoka LILUDISHE KWAO, oa mwingine atakayekuwa tayari kulea wanao.
 
Hivi wanawake wanaozungumziwa hapa ni hawahawa ninaowajua mie au kuna wengine? Kuna wanawake pasua kichwa sana bila makofi hawaelewi kabisa yaani hakuna kinachoenda. kiukweli saa nyingine ni bora kuwapuuzia tu vinginevo unaweza kujikuta umetanguliza mtu ahera. kuna wanawake wana mauzi sana (ila sio wote) na hawataki kunyooshwa na hapo ndo shida inapoanzia
 
Hapo kwenye sio wote ndio pazur
 
Back
Top Bottom