Tabia ya kufuta "x" kwenye nyumba hakuna adhabu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia ya kufuta "x" kwenye nyumba hakuna adhabu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgt software, May 13, 2011.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Hivi karibuni kumekuwepo tabia ya kufuta "X" kwenye nyumba zilizojengwa aidhakutokuwa na kibari au kuingilia barabara au kuejengwa sehemu isiyoruhusiwa.

  Mfano kuna sehemu amabzo barabara ya Bagamoyo Road inapopita hasa Tegeta wengi wameondoa X kwa kupigarangi upya, na pale Makumbusho kwenye Myumba ambayo ilikuwa iwe shule ya GreenAcre pamoja na geti la nyumba ya aliyekuwa waziri wa kilimo awamu ya Tatu Keenja , Saloon maarufu kona ya Mwananyamala nanyumba iliyovunjwa karibu na lango la Usarama wa Taifa ambalo limekuwa Hotel, Hivi vipimo hivi havipo sahihi au watu wanaichezea serikali.

  Hasara ya Kufuta X

  1. Uleta migongano ya kuuziananyumba zenye matatatizo kinyemela.

  2. Huleta matatizo makubwa kwa wapangaji wapya maana wanaingia bila kujua alafu wakati wa kuvunja wanapata hasara kubwa ya mali .

  3. Serikari inatumia Muda Mwingi kuweka vipimo halali alafu vinafutwa , tunapoteza muda wa kulipa wafanyakazi kwa hela za umma.

  4. usababisha uvunjifu wa Amani kati ya wapangaji wasiojua kuwa kuna matatizo dhidi ya wabomoaji wnaofuata sheria hivyo damu uweza kumwagika.

  Wizara ya Ardhi, Wizara ya Ujenzi pamoja na Halmashauri zote kuweni makini kwani serikali inapata hasara hata kwa kununua Rangi nyekundu.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hata huko Mbezi Beach Sykes Close kuna jamaa alikuwa anajenga sehemu bahari inapopumulia na halmashauri wakamuwekea "x" lakini kitu cha kushangaza jamaa alifuta ile "x" na akaendelea kujenga na karibu anahamia!!! Hawa jamaa wa halmashauri wako wapi?
   
Loading...