Tabia ya Kiasili ya 'Kijamaa' tuliyonayo Watanzania tunapokuwa nje ya nchi ina faida kwetu au inatufunga kimaarifa na kimaendeleo?

Kaka mkubwa Nyonzo bin Mvule safarini sauzi afrika.

Pole Sana kwa maswahibu, ila mshukuru Sana Mungu bado u hai.
Nashukuru ndugu yangu ila sijakuona siku mbili tatu,,, ndo kama hivyo kaka dunia uwanja wa fujo, yani walimwengu wasikuone unabadili mashati na kutomlilia mtu njaa, ukifanya hivyo tu wanajua una hela,,,
 
Mkuu pole sana na Binafsi Hisia Kali za Huruma na Huzuni huwa zipo karibu mno. Nikuombe tu basi usiendelee kuweka Picha zako zaidi za Majeraha kwani naumia.

Yawezekana Mwenyezi Mungu alikuwa na Makusudi yake Kwangu GENTAMYCINE nije na Uzi huu ambao utakuibua Wewe na uweze kutuambia yaliyokusibu huko.

Na Kinachoniuma waliotenda ni Wabongo.
Mkuu asante sana,, malipo hapa hapa duniani
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta na sikudhani kuwa huu Uzi wangu ungekuibua na hiki Kisa chako cha Ukweli mpaka kufikia Kujeruhiwa hivyo.

Mwenyezi Mungu akupiganie uweze kupona Jeraha lako hili ( hilo ) upesi na nakuomba sana usilipize Kisasi Shukuru tu upo Salama hivyo Hukumu Jadidi ( Kabambe ) dhidi yao ataitoa Yeye ( Mungu ) tena huenda ikawa ni Kubwa zaidi ya uliyokuwa ukitaka Kuitoa Wewe.
Nashukuru ndugu yangu tuko pamoja na sasa naendelea vizuri tu
 
Siko hapa JamiiForums kutaka Kushindana nami kama nilikuwa huko au naongopa.

Mwaka 2004 mpaka leo kukumbuka baadhi ya Maeneo pia nime jitahidi na ndiyo maana mingine sijaisahau.

Kukuonyesha kuwa nilikuwa na Kusoma hapo nakutajia niliosoma nao UCT hapo Beda ( sasa ni Lecturer University ), Mrs. Kibwana ( HR Stanbic jirani na Ubalozi wa Marekani ), Luhigo ( Mmoja wa IT Engineers wa Vodacom ) na Mrs. Musokwa ( aliyewahi kuwa Mmoja wa Marketing Executive wa Twiga Cement )

Na Apartment niliyokuwa naishi ni hilo Kubwa ( Pembeni ) hapo na hiyo Pick and Pay Supermarket ambapo kwa nyuma kuna Kituo cha Treni na mbele yake kidogo kuna Theatre Kubwa ya Utamaduni wa Mwafrika.

Namalizia tu kwa Kukuambia kwakuwa uko huko na najua unamjua Mtanzania aliyewekeza vyema huko aitwae Hamidu kuwa mwaka 2004 alimsindikiza nani Uwanja wa Ndege wa hapo Cape Town na akanituma baadhi ya Mizigo nimsaidie kumpelekea Kwao kwa Mama yake Mzazi Temeke.

Pumbavu...!!!

Hawa wote uliowaorodhesha hapa wametobowa maisha, wewe peke yako ndio umebaki kuwa tantalizer wa JF, jiangalie na ujitasmini unakosea wapi?
 
Wabongo ni watu wenye roho mbaya hasa linapokuja suala la maendeleo,,,, juzi tu nimepata majanga ya kuvamiwa na watanzania wenzangu wakishirikiana na wazawa kwa kudhani eti mimi tajiri,, kisa tu ni kuwa smart na kutomlilia mtu shida,

walionivamia wote nawajua so nauguza kwanza majeraha yangu kisha nami nitajua cha kufanya,,, ni bora kuishi kimpango wako unapokuwa nje kuliko kujichanganya na wabongo.

View attachment 1971919
Mimi nimewahi kulizwa malakar SS nikaja kuokolewa na gari za UNHCR.
Pia ndugu zangu wa kitanzania waliniliza Kerk and nugget Jo'burg
 
Back
Top Bottom