Tabia ya Kiasili ya 'Kijamaa' tuliyonayo Watanzania tunapokuwa nje ya nchi ina faida kwetu au inatufunga kimaarifa na kimaendeleo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,071
2,000
Nimetembea nchi kadhaa (hasa za Afrika) na nikiri tu kuwa huko sijui Majuu (Ulaya na Marekani) sijafika bado na kama ni kufika Kwangu basi ni ama tu kupitia ITV Daima au Facebook, Instagram na Twitter pekee.

Kuna 'Katabia' nimekaona kwa Watanzania wengi wakiwa tu katika hizo Nchi na wakishafahamiana tu basi upesi sana wataanza Kujitenga na Wenyeji wa huko na Kuanza kuishi Kimakundi (Kimaskani) kila mara utadhani wapo Mbagala, Tegeta, Manzese na hapa Kwetu Tandale nilipo.

Hata hivyo tabia yetu hii nimekuwa nikiwasikia Wenyeji wakiisifia na Kutupongeza Watanzania kuwa tuna Upendo, Umoja na Ushirikiano tofauti na walivyo Wao ambapo ukiwa tu nje ya nchi utajijua Mwenyewe na Mungu wako wa FAITH (IMANI), LOVE (UPENDO) na MIRACLE (MIUJIZA)

Sasa GENTAMYCINE nauliza je, kuna Faida Kubwa (Kiuchumi, Kiubunifu na Kidiplomasia) kwa hii tabia yetu Watanzania tukiwa ama abroad au overseas au labda upesi sana tunatakiwa tuiache kwani huenda ndiyo ikawa Chanzo cha Kutuchelewesha ambako Wanaijeria, Wasenegali, Wakenya, Waganda, Wakongo na Warwanda waliopo huko hawako kama tulivyo?

Nitashukuru mkinijibu Kiumakini mno.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,071
2,000
Africa ya wapi ww umeishia hapahapa Tanzania acha kuji proud kwa kutunywesha chai...hata airport tu kwenda kupokea mgeni haujaenda....na kawe na uhakika umepanga chumba
Oya mwana acha Utani basi nililouliza nina haraka nalo Kimrejesho kwani nina 'observation' yangu nimeiona mahala.

Sipo Tanzania sasa na nipo hapa Mali anapotoka Kiungo Fundi na Mahiri wa Simba SC Saido Kanoute na wanasema kuwa huenda Simba SC kwa Kipaji chake Kikubwa na kama hatopigwa 'Misumari' na Wazawa ikamuuza ama Liverpool FC au PSG.
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,205
2,000
Kwanza GENTAMYCINE ujue WaTz wengi hawako vizuri kwa lugha katibu zote za ughaibuni. Sasa wanapokutana inakuwa ni nafasi ya kujifariji kwa mawasiliano (kiswahili).

Ujue lugha yetu hii nje ya mipaka yetu haina nafasi sana.

Pili WaTz wamechanganyikana makabila mengi mengi si sawa na hizo nchi nyingine ambazo utakuta kuna makabila makuu yanayohasimiana.

Kwa Tanzania hakuna kabila kubwa la kudunisha makabila mengine. Hivyo ni rahisi kujichukulia kama WaTz na si vinginevyo
 

TZ-1

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
748
1,000
ugenini ni ugenini na pia hayo yanatokn kwakuw wa Tz wengi hatuna desturi ya explore the world ourself ,

Mtu leo akitak kwend mwanza anamtafuta mwenyewe wakat inabidi aend na bajet zake alale gesti na kufanya utalii BILA kuwasumbua wa kina ndugu na jamaa .

NB:- si vbaja kujuan na watu wa Taifa lako wanauwezo wa kukupamsaada wa haraka na hata kukuungansh na ndugu Wengne tuliowaacha Tz ila sio vizuri kushindw kujiamin na kujichangany na jamii/watu wa taifa fulan katk Taifa lap
 

uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
6,241
2,000
Nimetembea nchi kadhaa (hasa za Afrika) na nikiri tu kuwa huko sijui Majuu (Ulaya na Marekani) sijafika bado na kama ni kufika Kwangu basi ni ama tu kupitia ITV Daima au Facebook, Instagram na Twitter peke...

Inapendeza sana kuendeleza undugu ukiwa nje; na unaitajika; swala la fursa ni binafsi haliwi la kimkakati, kila mtu kwa namna yake Ana mahusiano na wengine ya fursa, ila undugu weekend kule nyama Choma, ugali na Mbuzi etc ni muhimu sana.
 

Nyonzo bin mvule

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
846
1,000
Wabongo ni watu wenye roho mbaya hasa linapokuja suala la maendeleo,,,, juzi tu nimepata majanga ya kuvamiwa na watanzania wenzangu wakishirikiana na wazawa kwa kudhani eti mimi tajiri,, kisa tu ni kuwa smart na kutomlilia mtu shida,

walionivamia wote nawajua so nauguza kwanza majeraha yangu kisha nami nitajua cha kufanya,,, ni bora kuishi kimpango wako unapokuwa nje kuliko kujichanganya na wabongo.

20211011_172451.jpg
 

ERICK EBYAGO

Member
Oct 10, 2021
7
45
Kiuchumi lazima mtu akwame kwani UNATOKA BONGO KWENDA NJE TAFUTA, SASA MARA UKO NA KINA MUTA, NDIMBO, MATEMBO mawazo yale TU ya home, TAFUTA NA WENYEJI tumia na wa home..
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,592
2,000
Wabongo ni watu wenye roho mbaya hasa linapokuja suala la maendeleo,,,, juzi tu nimepata majanga ya kuvamiwa na watanzania wenzangu wakishirikiana na wazawa kwa kudhani eti mimi tajiri,, kisa tu ni kuwa smart na kutomlilia mtu shida,, walionivamia wote nawajua so nauguza kwanza majeraha yangu kisha nami nitajua cha kufanya,,, ni bora kuishi kimpango wako unapokuwa nje kuliko kujichanganya na wabongo View attachment 1971919
Pole mkuu ni wapi huko
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom