Tabia mbaya kumi zinazofanya ushindwe kuwa na akiba "savings"

gunner's

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
335
119
Sio lazima ujumbe huu uwe sahihi kwa 100%, lakini nadhani kuna mambo kadhaa ya kujifunza humu.

TABIA MBAYA KUMI ZINAZOFANYA USHINDWE KUWA NA AKIBA "SAVINGS"....HATIMAE UNAKOSA MTAJI WA KUFANYA MAMBO YAKO.

1. Unanunua nguo bila mpangilio.
Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2. Unanunua Viatu bila mpango.
Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.

3. Unatoa ofa bar bila mpango.
Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4. Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 1000 ili uchati na marafiki Fb au wasaap Huo ni ujinga. Badilika.

5. Unakopa hela banki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6. Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.

7. Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa Tu na maradiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!

8. Una michepuko inayokutegemea we we kwa kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu huzinduki. Badilika.

9. Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.

10. Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.

Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa kufanya vitu vikubwa endelevu.
Anza sasa...badilika.
 
Kwa mchakato wako nimeona naweza kusave 250.000 kila mwezi, ASANTE SANA
 
Japo siyo siasa LAKINI tunashukuru, haya ni mawazo ya kujenga. Jambo jingine ambalo ni muhimu kuongezea:

11. Usikimbilie kuanzisha miradi ambayo huna uhakika nayo, mara nyingi miradi ya kuiga. Fanya utafiti wa kutosha, na unaporidhika na kuamua kuanzisha mradi, wekeza pesa kiasi kidogo, ile tu ya kuuwezesha mradi usimame, na kisha pima maendeleo ya mradi wenyewe kabla hujaingiza pesa yote uliyo nayo.

12. Weka vigezo vya kukusaidia kutambua kama mradi ni viable or not. Ukiridhika kuwa mradi hauna faida, chukua maumuzi magumu ya kuufunga kabla haujakuingizia hasara kubwa lakini pia usiwe mwepesi wa kufunga mradi kama una jibu la kwa nini mradi haukutoa faida, na hicho kilichosababisha una uwezo wa kukitatua.
 
Mimi naona kama zinanihusu zote.
Ina maana inanipasa kubadili mfumo wangu wote wa maisha dah!
Sasa mambo ya ushkaji tips kule.
 
kaka!
Kwa kweli hii ni the "anecdote of the year"

yaani umetugusa wengi kwa ncha kali ......big up!!
 
62 Reactions
Reply
Back
Top Bottom