Msengapavi
JF-Expert Member
- Oct 23, 2008
- 8,751
- 7,535
Taifa la wafu na mwenye 'uhai' akiwaongoza atakavyo! Shit hole!Mmeyakubali na mtayakubali yote na mtayaishi hayo kwakuwa ninyi ni taifa la wajinga
Taifa la wafu na mwenye 'uhai' akiwaongoza atakavyo! Shit hole!Mmeyakubali na mtayakubali yote na mtayaishi hayo kwakuwa ninyi ni taifa la wajinga
Mkuu maneno ulioyaongea yameniingia sana moyoni uko vizuri, ingekuwa mimi ni raisi ningeuchukuwa huu ushauri murua.Salamu wana JF.
Kuna mambo yanaendelea na sasa yamekuwa ni tabia kwa mkuu wetu wa nchi, kwa maoni yangu, Rais JPM amejijengea tabia ambazo kwangu mimi naona hazikupaswa kufanywa na kiongozi mkuu wa nchi kama yeye.
Rais ni kiongozi mkuu wa nchi ambaye nadhani hapaswi kuonesha chuki hadharani dhidi ya jambo fulani, anapaswa kutumia lugha za kuiongozi hata kama amekerwa na jambo na sio kuonesha ghadhabu. Kuonesha tabia za kukasirika kasirika kila wakati kwa kiongozi wa juu kunapunguza ladha ya hadhi ya kiti cha uraisi.
Rais ni kiongozi mkuu wa nchi ambaye hapaswi kuwa mwepesi wa kutoa matamko kwa mambo mepesi na kuegemea upande hasa inapoonekana upande huo unavunja sheria za wazi zilizowekwa katika kuongoza mambo yetu.
Rais ni kiongozi mkuu wa nchi ambaye hapaswi kutoa lugha tata zinazoibua maswali na minunguniko, anapaswa kutoa kauli ya kujibu kero za wananchi na kauli hizo ziegemee uhalisia wa jambo na haki na kushughulikia kero ambazo majibu yake hayakwazani na sheria na maamuzi ambayo huko nyuma yalishafanyika kwa misingi ya haki ( to be a problem handler).
Rais ni kiongozi mkuu wa nchi ambaye hapaswi kuchochea ukinzani bali anapaswa kuwa tumaini pale kunapoibuka sintofahamu kwenye jamii na kwenye nchi
KWA NINI NIMESEMA HIVYO ?
Kwa maoni yangu rais JPM hafanyi vizuri katika maeneo yote hayo, Mara nyingi kunaibuka sintofahamu kwenye jamii juu ya jambo fulani, lakini mara tu atowapo neno basi sintofahamu na minunguniko inazidi mifano ya karibuni ni .
Uzalendo wa makinikia
Hali ngumu ya maisha na kauli za wapiga dili.
Kukosekana mshikamano na umoja na kauli za mimi sipangiwi. N. k.
Maeneo hayo na mengine Rais alitakiwa kuja na kauli ya kuwavuta watanzania wote( Impresive language) na sio kuanza kubeza na kutoa kauli za kuwagawa watu hasa kwenye ajenda ambazo zina maslahi ya Taifa. Hiki kinachoendelea sasa ni matokeo ya kukosekana weledi katika maeneo hayo na sasa jamii inamuona rais wetu kama mtu aliyekosa mwelekeo kumbe ni kukosekana vitu fulani fulani tu.
LAWAMA KWA WASAIDIZI.
Sijui kuna nini lakini inaonekana hawa wasaidizi wa Mh Rais bado hawajafanya kazi yao. Kwa nini makosa haya yanajirejea rejea kila wakati? Kwani huko nyuma ilikuwaje kwa hao marais waliopita ? Hatukutegemea kuteleza kwa kauli zaidi ya mara moja vyenginevyo itakuwa kuna tatizo mahali. Mimi nawalaumu hawa wasaidizi na kama kuna tatizo binafsi kwa JPM jambo ambalo mimi silikubali kwamba eti alivyo ndio lazima tuwe watanzania wote si kweli. Unapoongozwa na mfumo inabidi wewe ndio ufuate mfumo ulivyo. Hii taasisi mfumo wake siku zote haukubali kwenda shaghala baghala na kutoa mikauli ya mijadala na minunguniko si kweli .
Kwa nini hao wasaidizi wasijiuzulu kama JPM ana tatizo binafsi, ikiwa ni hivyo basi hao wasaidizi ndio wabinafsi.
Tabia ya mtu haipaswi kuwa mwenendo wa taifa na ndio maana tukawa na KATIBA, SHERIA, BUNGE na MAHAKAMA.
Tukisikiliza maoni tunaweza tukabadilika, kukataa mawazo ya wengine si mwarubaini wa kukubalika
Mungu ibariki Tanzania.
Kishada
Salute. Tunataka hoja kama hizi .Chifu, nakubaliana na hoja yako ya msingi. Ila nimeona nichangie kidogo kwenye hilo la wasaidizi na washauri wa Rais. Kuna mambo mawili hapa. Moja, Katiba ya JMT, sura ya 37(1) inasema hivi: "Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote." Kwa hiyo Rais Magufuli anavyosemaga yeye asikilizi ushauri wa mtu yeyote, yupo sawa, kwani Katiba inamruhusu. Tatizo hapa ni Katiba yetu mbovu.
Pili, kwenye public service, haswa miongoni mwa wanasiasa na watumishi wengine waandamizi, hakuna utamaduni wa kujiuzulu. Hili ni tatizo kubwa sana. Na ndilo linamtafuna hata Magufuli ambaye kila siku anasema anajua jinsi nchi hii ilivyochezewa kwani amekuwa serikalini zaidi ya miaka 20. Ukiwauliza wapiga vigelegele wake, ilikuwaje sasa akaangalia tu nchi ikichezewa? Wanamtetea hakuwa na madaraka. Ukiwauliza, kwanini sasa hakujiuzulu ili kuonyesha kutokukubaliana na uchezewaji wa nchi? Wanakosa jibu! Umesema wazi, ubinafsi nao ni tatizo kubwa. Yaani mtu anaona hali mbaya kwenye uongozi serikalini, lakini akifikiria kujiuzulu na jinsi ambavyo familia yake itapata shida, anaamua kuweka mkia nyuma na kuangalia tu nchi ikiangamia.
Nina wasiwasi na akili zakoshi
shida ya watanzania walio wengi ni unafiki...Magufuli kanyaga mafuta twende kazi wanaopiga kelele ama wameathirika moja kwa moja au ni ndugu zao wale wa vyeti feki wewe chapa kazi usisikilize kelele ziwe za mtandaoni, magazeti, maasikofu au nani. Kimsingi Mheshimiwa Rais wewe ni Rais Bora kuwahi kutokea Tanzania. Mungu akubariki sana wewe chapa kazi usithubutu kurudi nyuma ukirudi nyuma utakuwa umekosea sana...
mimi sina wasiwasi na akili zako hata kidogoNina wasiwasi na akili zako