Tabia hizi mbili za Hayati Magufuli zilifuta Mazuri yake Mengi sana, Watanzania kuna la kujifunza hapa

Zilifuta mazuri yake kwenu ila kwa sisi wengine bado yupo anaishi ndani yetu
Nchi ilijawa na manyang'au, JPM anaingia ikulu nchi haina pesa hata ya kuongozwa kwa zaidi ya siku 9, yalitegemea angejificha kwenye upumbavu wa democracy uliotusababishia tuendelee kuwa maskini tegemezi kwa mabeberu hadi leo hii ilihali tuna kila aina ya utajiri wa rasilimali?
 
Hilo pimbi lilipitia malezi mabaya ndo maana lilikuwa hivyo

Wazazi tuzingatie kuwapatia watoto wetu malezi mazuri yakujari utu
Ni kweli ila pimbi zaidi ni wewe ambaye hukuweza kumwona akiwa katika uwaziri zaidi ya miaka 20, hadi aliposhika Urais akaanza kukulipisha kodi bila janja janja za kukwepa, kutumbuliwa kwa vyeti feki, madawa ya kulevya, ufisadi na kukukwamisha usitoroshe wanyama kwenda nnje ya nchi.
 
Hii "Lakini" jisemee wewe mwenyewe usituhusishe sisi wananchi wazalendo wa ukweli TZ.
Sijisemei mwenyewe. Tuko wazalendo wengi kweli wanaoipenda nchi yetu. Magufuli alikuwa na nia nzuri sana na nchi yetu na angeweza kuwa mmoja wa marais bora kabisa lakini upeo wake wa kuona mambo ulikuwa mdogo. Kuna makosa aliyofanya ambayo yalikuwa grave mistake.
 
Mimi nilimshusha tu alipoacha kutupandisha madaraja na kutuongezea mishahara! kwa sababu ya kununua ndege, kujenga flyovers, nk.

Halafu wakati huo huo akapandisha makato ya bodi ya mikopo kutoka 8% mpaka 15%!! Hakika maisha ya watumishi wengi wa umma yalikuwa ni magumu sana wakati wa utawala wake.
Ugumu wa maisha na ulaisi wa maisha ni akili ya mtu mwenyewe wewe endelea kubweteka na kutegemea uongezewe mshahara Pana watu hawana mishahara lakini mambo Safi.
 
Nadhani kuna jambo lingine tofauti na unalofikilia ila ukweli ndio ule nilioandika mwanzo.
Ni upotofu wako tu. 1. Alishindwa kuona (wakati asilimia kubwa ya watu tulishaona) kuwa wale watu waliokuwa wanamsifia sana walikuwa wanamsifia kinafiki ili matumbo yao yajae na wale waliokuwa wanamkosoa (ambao alikuwa anawaona ni maadui)walikuwa wanamtakia uongozi bora.
2. Alishindwa kuona madhara ya kuingilia uchaguzi wa bunge na kuweka wabunge vilaza wasio na sifa. Kweli hakujui Nchi inahitaji muhimili wa bunge wenye watu competent?
3. Alikuwa anateua watu wabovu na waovu ili mradi tu wanamsifia na kufukuza wenye akili na hekima kisa wamesema ukweli.
4. Aliamini kwenye kuua watu wenye msimamo kinzani
5. Hakupenda uwazi na uhuru kwenye vyombo vya habari na hata serikali yake ilikuwa inafanya makosa mengi na kuchukuwa mikopo kwa kificho.
6. Alishindwa kuona kuwa hata kama atafanya vizuri namna gani lakini asiwepoweka mfumo wa uongozi madhubuti ni siku akiwa hayupo kila kitu kitarudi kama tulivyokuwa.
 
Kila binadamu anayomapungufu tena mengi hayo ya magufuri ndo uliyoyaona embu na wewe tupe mapungufu yako nayo ya weke hapa.bora hata huyo unae msema huwenda yeye akawa nafuu zaidi yako.
Hizi argument zako ni za watu ambao hawajaenda shule na kuwa na upeo wa kuona na kuchambua mambo ya maisha. Mimi nilidhani wazee wa vijijini wasio na elimu ndiyo wangekuwa wanasema hivi. Unajua maana ya kuwa kiongozi? Huyu unayemwambia akupe mapungufu yake aliwahi kuwa rais wa Tanzania? Hujui wataalam, kutokana na uzoefu walifanya rais awe na washauri, wataalam na kila aina ya usaidizi plus mihimili mingine ya utawala ili kufanya nchi isiongozwe na kichwa cha mtu mmoja? Anapoingia rais ambaye anaweka juhudi kwenye kubomoa ile misingi bora ya utawala ili yeye ndiye awe muamuzi wa kila kitu huoni hapo kuna shida kubwa?
 
Habari wana JF, kwenye hii dunia hakuna mtu alie kamilika nna maana kila mtu ana tabia au vijitabia ambavyo watu wengine hawavipendi au vinakufanya mtu kufanya ufanya mambo isivyo.

Hivyo Pia JPM pamoja na mazuri yake yote yanayomfanya aonekana ni Rais bora mpaka alikuwa na tabia mbili kubwa ambao kwa namna moja au nyingine zilimpotezea ubora wake :-
1.Mtu wa Visasi ,kwenye hii Dunia kila siku tunakosana na kutofautiana na watu wengi sana katika Haya wengi husamehe wengine hawawezi hivyo hutulia na kusubiri muda muafaka wa kulipa visasi.

Kiongozi watu aliweza kulipa visasi kwa vikundi mpaka kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja ,kuna watu walikuwa maskini ,Nchi waliiona Chungu kwa sababu za visasi tu ,kwamba nlikuwa sina mamlaka sasa ninao mtakoma ,hii tabia iliharibu sana Nchi na ndio watu walisema ukatili.

2.Hakuwa Muwazi ,Katika Uongozi kuna mambo unaweza waficha wananchi wako lakini Mambo yanayo husu Maendeleo yao ni bora tukajua ,Tulikopa sana ,Tulipewa misaada Mingi ,tulipewa Pesa za COVID-19 ,kuna hela zilikusanya kwa Nguvu zikiwemo za madeni ya Nyuma kutoka kwa Matajiri na watu kama kina Sabaya na kwenda kufanya maendeleo bila watanzania kujua .
Mambo haya yote watanzania ilibidi wajue ,ili hata tunavyo ambiwa Deni la Taifa ni Trilioni 70 tunaelewa sio kuficha Taarifa .
Hivyo watanzania visasi havifai mtu ulikosana nae Darasani ,ukiwa Waziri ,JF ukipata Cheo kikubwa zaidi Tusahau na kusonga mbele .
Lakini mbali na mapungufu hayo makibwa mawili bado JPM ni mfano wa kuigwa kwa wazalendo wote aliipenda sana Tanzania .
Visasi na Kutokuwa Muwazi sio sifa nzuri kwa kiongozi .
Alishasema ana mazuri na mabaya yake hamkumwelewa tu?vichwa vimekua vigumu

Watz walishamuelewa,maisha yanaendelea
 
Nyie mnachanganya Mambo..watu wakiwa wananyooshwa warudi kwenye mstari nyie mnaita eti visasi..binadamu mna shida sana...waswahili wanasema samaki mkunje bado mbichi..Sasa masamaki mengine yalishaachwa yakakomaa, unadhani utayakunjaje....lazima utumie nguvu ya wastani lasivyo hutayaweza..acheni kulalama..wananchi walitaka Rais wa namna hiyo kipindi hicho
Na kupola maduka ya kubadilishia fedha ,Nayo ilikuwa kuwarusisha watu kwenye msitari?
 
Hata mimi mtu wa Visasi,Yaani unifanyie jambo Utegemee Nikusamehe..Hiyo sio kazi yangu kusamehe!!! Lazima nikulipize kama jambo hutaki kufanyiwa na wewe Usimfanyie mwenzako kwani we nani??
Bora umesema! Majitu mengine mapuuzi kweli. Sina chapaa, sina umaarufu. Eti kwa kuwa wewe maarufu unidhalilishe kwa pesa zako utegemee nami nikishika mamlaka nikusamehe? ***** nakula utumbo aisee..

Rejea kisa cha Babu Seyyer na Msoga... Baboo Seyyer alikuwa na hela na chapaa, wakati huo Msoga hana ubavu wa kushindana na Baboo Seyyer mzee wa town. Alimdhalilisha na kumfanyia dharau.

Ila Msoga alopopata madaraka...
 
Nchi ilijawa na manyang'au, JPM anaingia ikulu nchi haina pesa hata ya kuongozwa kwa zaidi ya siku 9, yalitegemea angejificha kwenye upumbavu wa democracy uliotusababishia tuendelee kuwa maskini tegemezi kwa mabeberu hadi leo hii ilihali tuna kila aina ya utajiri wa rasilimali?
Wahuni siyo watu yaani amekuta hela ya kuongozea nchi siku tisa??? Msoga alizingua sana
 
Habari wana JF, kwenye hii dunia hakuna mtu alie kamilika nna maana kila mtu ana tabia au vijitabia ambavyo watu wengine hawavipendi au vinakufanya mtu kufanya ufanya mambo isivyo.

Hivyo Pia JPM pamoja na mazuri yake yote yanayomfanya aonekana ni Rais bora mpaka alikuwa na tabia mbili kubwa ambao kwa namna moja au nyingine zilimpotezea ubora wake :-
1.Mtu wa Visasi ,kwenye hii Dunia kila siku tunakosana na kutofautiana na watu wengi sana katika Haya wengi husamehe wengine hawawezi hivyo hutulia na kusubiri muda muafaka wa kulipa visasi.

Kiongozi watu aliweza kulipa visasi kwa vikundi mpaka kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja ,kuna watu walikuwa maskini ,Nchi waliiona Chungu kwa sababu za visasi tu ,kwamba nlikuwa sina mamlaka sasa ninao mtakoma ,hii tabia iliharibu sana Nchi na ndio watu walisema ukatili.

2.Hakuwa Muwazi ,Katika Uongozi kuna mambo unaweza waficha wananchi wako lakini Mambo yanayo husu Maendeleo yao ni bora tukajua ,Tulikopa sana ,Tulipewa misaada Mingi ,tulipewa Pesa za COVID-19 ,kuna hela zilikusanya kwa Nguvu zikiwemo za madeni ya Nyuma kutoka kwa Matajiri na watu kama kina Sabaya na kwenda kufanya maendeleo bila watanzania kujua .
Mambo haya yote watanzania ilibidi wajue ,ili hata tunavyo ambiwa Deni la Taifa ni Trilioni 70 tunaelewa sio kuficha Taarifa .
Hivyo watanzania visasi havifai mtu ulikosana nae Darasani ,ukiwa Waziri ,JF ukipata Cheo kikubwa zaidi Tusahau na kusonga mbele .
Lakini mbali na mapungufu hayo makibwa mawili bado JPM ni mfano wa kuigwa kwa wazalendo wote aliipenda sana Tanzania .
Visasi na Kutokuwa Muwazi sio sifa nzuri kwa kiongozi .
Nice try but a desperate deceptive spin, obviously. Attempting a fond explanation of a really twisted character is never easy.
 
Na kupola maduka ya kubadilishia fedha ,Nayo ilikuwa kuwarusisha watu kwenye msitari?

Unataarifa za watu kusafirisha pesa nje na kupokea pesa za nje bila kulipa Kodi ya serikali?

Haya Leo yamerudi tena na Kodi hazilipwi tena ktk Miamala wanayofanya.

Leo watu wanafanya biashara hata ya 900 millions na hawalipi Kodi hata senti serikalini.

Tujiandae wanainchi kulipa kodi hadi za kuku na mbuzi wetu tunaowafuga majumbani,

Serikali itapataje pesa kama haisimamii ulipwaji wa Kodi vizuri?

Uzuri wa Magufuli alimwaga vijana wengi TISS mitaani.
alijuwa alitendalo.,
 
Back
Top Bottom