Tabia hizi mbili za Hayati Magufuli zilifuta Mazuri yake Mengi sana, Watanzania kuna la kujifunza hapa

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,100
1,814
Habari wana JF, kwenye hii dunia hakuna mtu alie kamilika nna maana kila mtu ana tabia au vijitabia ambavyo watu wengine hawavipendi au vinakufanya mtu kufanya ufanya mambo isivyo.

Hivyo Pia JPM pamoja na mazuri yake yote yanayomfanya aonekana ni Rais bora mpaka alikuwa na tabia mbili kubwa ambao kwa namna moja au nyingine zilimpotezea ubora wake :-
1.Mtu wa Visasi ,kwenye hii Dunia kila siku tunakosana na kutofautiana na watu wengi sana katika Haya wengi husamehe wengine hawawezi hivyo hutulia na kusubiri muda muafaka wa kulipa visasi.

Kiongozi watu aliweza kulipa visasi kwa vikundi mpaka kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja ,kuna watu walikuwa maskini ,Nchi waliiona Chungu kwa sababu za visasi tu ,kwamba nlikuwa sina mamlaka sasa ninao mtakoma ,hii tabia iliharibu sana Nchi na ndio watu walisema ukatili.

2.Hakuwa Muwazi ,Katika Uongozi kuna mambo unaweza waficha wananchi wako lakini Mambo yanayo husu Maendeleo yao ni bora tukajua ,Tulikopa sana ,Tulipewa misaada Mingi ,tulipewa Pesa za COVID-19 ,kuna hela zilikusanya kwa Nguvu zikiwemo za madeni ya Nyuma kutoka kwa Matajiri na watu kama kina Sabaya na kwenda kufanya maendeleo bila watanzania kujua .

Mambo haya yote watanzania ilibidi wajue ,ili hata tunavyo ambiwa Deni la Taifa ni Trilioni 70 tunaelewa sio kuficha Taarifa .

Hivyo watanzania visasi havifai mtu ulikosana nae Darasani ,ukiwa Waziri ,JF ukipata Cheo kikubwa zaidi Tusahau na kusonga mbele .
Lakini mbali na mapungufu hayo makibwa mawili bado JPM ni mfano wa kuigwa kwa wazalendo wote aliipenda sana Tanzania .
Visasi na Kutokuwa Muwazi sio sifa nzuri kwa kiongozi .
 
Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
11,224
15,316
Mama Samia hana hizo tabia je Tanzania ipoje sasa? Jk pia hakuwa na hizo tabia nchi alifikishaje? Unajaili vitu vya ovyo ovyo Watanzania wengi wanataka maendeleo bila kujali wana raisi wa aina gani na ndio maana ukimuondoa Mwalimu Nyerere anayefuata kwa kukubalika ni Magufuli hivo vitu ulivyoandika wewe ndio vinaangaliwa na wenye itikadi ya vyama na wanasiasa wenzake ila kwa sisi ambao hatuna itikadi ya vyama tunaangalia utendaji wa mtu na namna anavyofanya maendeleo.
 
MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
3,851
6,840

Diamondo anatukanwa huko celebrity. Cheupe uko huku unafanya uchawa kwa maiti
 
Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
1,774
3,346
Habari wana JF, kwenye hii dunia hakuna mtu alie kamilika nna maana kila mtu ana tabia au vijitabia ambavyo watu wengine hawavipendi au vinakufanya mtu kufanya ufanya mambo isivyo.

Hivyo Pia JPM pamoja na mazuri yake yote yanayomfanya aonekana ni Rais bora mpaka alikuwa na tabia mbili kubwa ambao kwa namna moja au nyingine zilimpotezea ubora wake :-
1.Mtu wa Visasi ,kwenye hii Dunia kila siku tunakosana na kutofautiana na watu wengi sana katika Haya wengi husamehe wengine hawawezi hivyo hutulia na kusubiri muda muafaka wa kulipa visasi.

Kiongozi watu aliweza kulipa visasi kwa vikundi mpaka kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja ,kuna watu walikuwa maskini ,Nchi waliiona Chungu kwa sababu za visasi tu ,kwamba nlikuwa sina mamlaka sasa ninao mtakoma ,hii tabia iliharibu sana Nchi na ndio watu walisema ukatili.

2.Hakuwa Muwazi ,Katika Uongozi kuna mambo unaweza waficha wananchi wako lakini Mambo yanayo husu Maendeleo yao ni bora tukajua ,Tulikopa sana ,Tulipewa misaada Mingi ,tulipewa Pesa za COVID-19 ,kuna hela zilikusanya kwa Nguvu zikiwemo za madeni ya Nyuma kutoka kwa Matajiri na watu kama kina Sabaya na kwenda kufanya maendeleo bila watanzania kujua .
Mambo haya yote watanzania ilibidi wajue ,ili hata tunavyo ambiwa Deni la Taifa ni Trilioni 70 tunaelewa sio kuficha Taarifa .
Hivyo watanzania visasi havifai mtu ulikosana nae Darasani ,ukiwa Waziri ,JF ukipata Cheo kikubwa zaidi Tusahau na kusonga mbele .
Lakini mbali na mapungufu hayo makibwa mawili bado JPM ni mfano wa kuigwa kwa wazalendo wote aliipenda sana Tanzania .
Visasi na Kutokuwa Muwazi sio sifa nzuri kwa kiongozi .
Huu uandishi wako unachosha sana kusoma jifunze kuandika vizuri
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
18,759
51,880
Mimi nilimshusha tu alipoacha kutupandisha madaraja na kutuongezea mishahara! kwa sababu ya kununua ndege, kujenga flyovers, nk.

Halafu wakati huo huo akapandisha makato ya bodi ya mikopo kutoka 8% mpaka 15%!! Hakika maisha ya watumishi wengi wa umma yalikuwa ni magumu sana wakati wa utawala wake.
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,454
3,100
Kutomridhisha kila mtu ni sawa, ila visasi haipaswi kuwa hulka ya kiongozi wa nchi ya kidemokrasia.
Nyie mnachanganya Mambo..watu wakiwa wananyooshwa warudi kwenye mstari nyie mnaita eti visasi..binadamu mna shida sana...waswahili wanasema samaki mkunje bado mbichi..Sasa masamaki mengine yalishaachwa yakakomaa, unadhani utayakunjaje....lazima utumie nguvu ya wastani lasivyo hutayaweza..acheni kulalama..wananchi walitaka Rais wa namna hiyo kipindi hicho
 
RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,100
1,814
Nyie mnachanganya Mambo..watu wakiwa wananyooshwa warudi kwenye mstari nyie mnaita eti visasi..binadamu mna shida sana...waswahili wanasema samaki mkunje bado mbichi..Sasa masamaki mengine yalishaachwa yakakomaa, unadhani utayakunjaje....lazima utumie nguvu ya wastani lasivyo hutayaweza..acheni kulalama..wananchi walitaka Rais wa namna hiyo kipindi hicho
Alikuwa kiongozi mzuri lakini mapungufu hayakosekani
 
32 Reactions
Reply
Top Bottom