Tabia hii ya kutupa maiti za wahamiaji haramu katika mto Ruvu ni Aibu kubwa kwa Taifa letu.

Bhampupile

JF-Expert Member
Jul 6, 2015
813
1,000
Habari hii ya maiti kutupwa ndani ya mto Ruvu imeelezezwa vzr sn katika gazeti la Mwananchi leo 17.12.2016.

Ni habari ya kusikitisha kwamba Zawadi tuliyopewa na Mungu ya mto huu sisi tunaugeza kuwa ni kaburi la kuwazikia wananchi wa Ethiopia na Somalia.

Wakazi waishio karibu na mto huu wanasema imekuwa ni kawaida kwao kuona mifuko ya sandarusi ikielea juu ya maji ikiwa na miili ya wahamiaji haramu ndani yake.
Ni habari ya kusikitisha na ya kulitia Aibu taifa letu.

Tunajiuliza hawa watu wanaofanya hii DILI la wahamiaji haramu kweli serikali imewashindwa kabisa hawa Wapiga DILI hili? Maana si Mara ya kwanza hawa was Ethiopia na wa Somali kukutwa wamekufa kwa wingi na wengine kutelekezwa maporini,,

kuna wakati roli lilikamatwa limepakia watu hawa ndani likiwa na chokaa., pia walikutwa maiti wengi humo ndani ya hilo roli,, kuna wakati mwingine wanakijiji kule Singida walikuta kundi kubwa la Waethiopia na Wasomali likitoka vichakani na kuvamia mashamba yao kujipatia chochote,, hatimaye wakawakamata pamoja na Fuso liliowabeba na dereva wao na kuwakabidhi polisi.

Na sasa hv tena wapiga DILI hawajaacha tabia yao wamebeba Wahamiaji haramu 87 na maiti zao kuzitupa mtoni..maji wanayotumia wananchi yamegeuzwa ndiyo kaburi la Wageni.

Wanafikaje hawa Bagamoyo na Singida? Na wakati mwingine hukamatiwa Mbeya.
TANZANIA YETU NZR YENYE MITO NA MAZIWA SISI TUNAGEUZA MAJI YETU KUWA KABURI LA WAGENI? Aibu Kubwa
 

dyngrey

New Member
Dec 17, 2016
2
20
Bado hawajatoa ufafanuzi ni za kina nani hivyo hatuwezi kurupuka ni za wa ethiopia au somali....
 

Small Axe

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
649
500
Mbona una conclude kua ni wa hamiaji haramu una uwakika gani?? watu wanao potea wanao tangazwa kwenye vyombo vya habari..haijulikan wanaendaga WAP nadhani tungeanza Ku suspect kwa hawa lkn sio moja kwa moja kuhisi wa maifa ya mbali bila kua na uhakika..tatizo nchi yetu haiamini research Bali gossip
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom